Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 15 November 2013

MUUAJI NA MBAKAJI ANYONGWA BAADA YA KULA PIZZA NA KUKU


MFUNGWA katika gereza la Florida, ambaye alihukumiwa kunyongwa kwa makosa ya ubakaji na mauaji ya msanii mwaka 1991, ameuawa Jumatatu jioni.
Darius Kimbrough, ambaye alikuwa na miaka 18 wakati alipovunja na kuingia nyumbani kwa Denise Collins na kumshambulia wakati akiwa amelala, alitangazwa kwamba amekufa majira ya saa 12.18 jioni baada ya kudungwa sindano za sumu.
Saa kadhaa kabla ya kuuawa – likiwa ni tukio la pili jimboni Florida la kuwaua kwa sumu wafungwa waliohukumiwa kunyongwa - Kimbrough alitembelewa na familia yake na rafiki zake.
Kimbrough aliyekuwa na miaka 40, ambaye alihukumiwa mwaka 1994 kwa kitendo cha unyama, aliomba apewe chakula cha mwisho, ambacho alikula kabla ya saa 3.45 asubuhi.
Miongoni mwa vikorokoro alivyoomba kula ni pamoja na vipande viwili vya pizza, nyanya za kukaanga, kuku wa kuchoma, ice cream na matunda.
Mama yake, shangazi zake watatu na binamu yake walikuwa miongoni mwa wageni wa mwisho waliomtembelea, msemaji wa Idara ya Urekebishaji Tabia (Department of Corrections) Jessica Cary aliliambia Orlando Sentinel.
Kimbrough alitumikia miaka 19 gerezani kwa mauaji, ubakaji na ujambazi.
Alihukumiwa kwa kumshambulia Collins (28) baada ya vipimo vya DNA kutoka katika mbegu za kiume zilizotokana na ubakaji alioufanya kubainika miezi mitano baadaye kwa kuthibitishwa na vielelezo vilivyopatikana kwenye nyumba ya mwanamke huyo.
Kimbrough alipanda hadi ghorofa ya pili alikokuwa akiishi mwanamke huyo na kumshambulia katika chumba cha kulala. Taya na fuvu lake mwanamke huyo vilikuwa vimevunjika na akafariki siku iliyofuata akiwa hospitalini.
Ndugu wa Bi Collins walihudhuria wakati Kimbrough akiuawa.

Chanzo: dailymail.co.uk

No comments:

Post a Comment