Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 16 November 2013

AMCHOMA VISU MUMEWE, KISA HAKUMPIGIA SIMU!

MWANAMKE mmoja mwenye miaka 21 alimchoma visu mchumba wake kwa sababu alishindwa kumpigia simu kila baada ya saa mbili wakati alipokwenda kujirusha, akamuacha na majeraha makubwa ambayo madaktari walihisi amekufa, mahakama ya Uingereza iliambiwa wiki hii.
Rhiann Burnie, 21, alimtandika mchumbaake Shane McMullen, 23, ambaye ni mpanga tofali, kisha akamchoma visu vya haja begani kabla ya kuwasha sigara na kufuta damu huku akimuacha amelala sakafuni akipigania uhai wake, mahakama ya Burnley Crown Court ilielezwa.
Upande wa mashtaka ulidai kwamba mwanamke huyo alipandwa na hasira baada ya mwandani wake huyo kwenda kujirusha akimwacha nyumbani na binti yao mwenye miaka miwili.
Pamoja na jeraha kubwa lililotokana na kukatika kwa mshipa wa ateri na kusababisha kupoteza damu nyingi, McMullen alinusurika kifo lakini amepoteza kumbukumbu na anapatwa na ndoto za ajabu za kuchomwa kisu tena.
Mahakama iliambiwa kwamba alijeruhiwa kwa kuwa tu alisahau kumpigia simu mchumba wake huyo ‘kila baada ya saa mbili’ kama mwanamke huyo alivyotaka.
Mahakama ya Burnley Crown Court iliambiwa wawili hao walikuwa kwenye uhusiano kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo mwanzoni mambo yalikuwa swafi lakini ghafla roho ya kinyama ya Burnie ikaibuka, alisema mwendesha mashtaka, Rachel Woods.
Burnie alikuwa amejaribu mara mbili huko nyuma kumshambulia kwa kisu McMullen.
Pia kila wakati alikuwa akivunja milango na samani za ndani kila walipokuwa wakigombana.
Mpo hapo?

No comments:

Post a Comment