Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 5 November 2013

WAAJIRI WATAKIWA KUWAELIMISHA WAFANYAKAZI KABLA YA KUSTAAFU

 Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maazimo yaliyofikiwa kwenye mkutano wa 23 wa wanachama na wadau wa mfuko huo uliofanyika Arusha Oktoba mwaka huu ambapo moja ya maazimio ni waajiri kuwapa fursa wafanyakazi wao kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii. Katikati ni Meneja Uwekezaji wa mfuko huo Selestine Some na Mwishoni ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Fatma Salum.
 Meneja Huduma kwa Wateja na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Godfrey Mollel akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) mpango wa mfuko huo kufikisha wanachama 400,000 ifikapo mwaka 2015, kwa sasa mfuko huo una wanachama takribani 300,000, kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano na Mfuko wa Pensheni wa PPF katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jana Jumatatu jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Silayo - MAELEZO

Na Hassan Silayo - Maelezo

Waajiri nchini wametakiwa kuwa utaratibu wa kutoa mafunzo elekezi kwa waajiriwa kuhusu namna ya kujiandaa na maisha ya kustaafu tangu siku mfanyakazi anapoingia katika ajira.
Wito huo umetolewa na Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) Lulu Mengele wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana Jumatatu jijini Dar es Salaam.
Megele alisema kuwa kumekuwa na tabia ya waajiriwa kusahau kujiwekea akiba na hivyo kusababisha matatizo wakati wa kustaafu.
“Napenda kuwaasa waajiri waanzishe utaratibu wa kutoa mafunzo elekezi kuhusu namna ya kujiandaa na maisha ya kustaafu tangu siku mfanyakazi anapoingia katika ajira hii itamsaidia mfanyakazi kuwa na mipango ya maandalizi kabla ya kustaafu na sio kusubiri mtu astaafu ndio aanze kuweka mipango ya maisha yake,” Alisema Mengele.
Pia Menegele aliongeza kuwa kuna haja ya waajiri nchini kuwapa fursa Wafanyakazi wapya kujiunga na Mifuko mbalimbali ya Hifadhi ya Jamii.
“Napenda kuwaasa waajiri wote nchini kuwapa fursa wafanayakazi wapya kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwani kwa kufanya hivi kutaweza kuwasaidia wafanyakazi kuwa na uwezo wa kujikimu na kukabiliana na changamoto za maisha katika siku za baadae,” alisema.
Akieleza mipango ya kuongeza wanachama meneja wa huduma kwa wateja na wanachana Godfrey Mollel alisema wanamipango ya kuongeza wanachama hadi kufikia 400,000 ifikapo mwaka 2015.
“Kwa sasa tuna wanachama 300,000 lakini kutokana na ubora wa huduma za PPF tunategemea kuongeza idadi ya wanachama hadi kufikia 400,000 ifikapo mwaka 2015.
Mfuko wa Pensheni wa PPF unajivunia kutekeleza majukumu yake kwa asilimia 80 kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mwasiliano (TEHAMA).

No comments:

Post a Comment