MUDHIHIR MOHAMMED
MUDHIHIR
Mbunge wa zamani wa
Mchinga. Elimu ya msingi aliipata katika shule za Mchinga (1958 hadi 1959),
Msinjahili (1959 hadi 1961) na Mangamba Middle School (1962 hadi 1965) kabla ya
kujiunga na shule ya sekondari Lindi (1966 hadi 1969). Baadaye akajiunga na
Chuo cha Ualimu Marangu kwa mafunzo ya Cheti cha Ualimu Daraja A (1973 hadi
1974). Kati ya mwaka 1981 na 1982 alisoma kidato cha tano na sita katika shule
ya Kujitegemea (Private School). Mwaka 1988 na 1989 alihitimu Cheti cha Sheria
katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwaka 2000 alijiunga na masomo ya shahada
ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Washington, Marekani lakini hakumaliza.
Kati ya mwaka 1970 na
1973 alikuwa Msaizidi wa Usajili katika Wizara ya Elimu. Mwaka 1975 hadi 1981
alikuwa Mwalimu Daraja la Tatu A. Kuanzia mwaka 1981 hadi 1995 alikuwa Ofisa
Usalama wa Taifa, kipindi ambacho pia alikuwa Mkuu wa Chuo cha Usalama wa Taifa
cha Zanzibar. Mwaka 1997 hadi 2005 alikuwa Naibu Waziri wa Kazi, Maendeleo ya
Vijana na Michezo.
Alikuwa anamiliki bendi
yake ya muziki wa dansi ya Mchinga Sound, lakini ikamshinda kuiendesha.
JOHN SULLIVAN
John Sullivan (John A.
Sullivan) alizaliwa Ijumaa, Januari 01, 1965 mjini Tulsa, Oklahoma nchini
Mrekani. Ni mwanasiasa maarufu Mkatoliki huko Marekani. Baba yake ni Daniel na
mama yake ni Mag. Kwa kuzaliwa Januari Mosi, nyota yake ni Mbuzi (Capricon).
John Sullivan alisoma
katika shule ya Bishop Kelley High School, Tulsa, Oklahoma na akapata shahada
yake ya kwanza ya utawala katika biashara (BBA) katika Chuo Kikuu cha Northeastern
State University, Tahlequah, Oklahoma mwaka 1992.
Mkewe anaitwa Judy Beck.
COLIN MORGAN
Mwigizaji huyu wa runinga alizaliwa Januari Mosi, 1986 huko Ireland
Kaskazini na nyota yake ni Mbuzi (Capricon).
Kwa wafuatiliaji wa tamthiliya za runinga, lazima wanamfahamu Colin
Morgan, kijana aliyejipatia umaarufu mkubwa kwenye tamthiliya ya Merlin
iliyokuwa ikirushwa na BBC.
Kabla ya kuwa maarufu alisoma shule ya muziki na maigizo ya Royal
Scottish Academy. Ameshiriki filamu za Island (2011) na Parked (2010). Kaka yake anaitwa Neil.
MORRIS CHESTNUT
Staa huyu wa maigizo ya runinga alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1969
huko California.
Anafahamika zaidi kutokana na ushiriki wake katika filamu iliyoteuliwa
kuwania tuzo za Oscar ya Boyz in the Hood, ambapo alishiriki kama Visitor
Ryan.
Wakati
akiwa chuo alikuwa mwanachama wa Phi Beta Sigma.alimuoa Pam
Byse mwaka 1995. Ameshiriki pia filamu ya Under
Siege 2: Dark Territory akiwa na Steven Seagal, na filamu yake ya kutisha ya Half
Past Dead.
JACK WILSHERE
Mchezaji wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya England ambaye
alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1992. Ametimiza miaka 23.
Wilshere
alijiunga na klabu ya Arsenal mwaka 2008 na mwaka 2010 akaitwa kwenye timu ya
taifa ya England. Wakati anajiunga na ‘Wapiga Bunduki wa London, alitokea
kwenye timu ya vijana (Academy) ambako alijiunga tangu akiwa na miaka 9.
Alianza
kuiwakilisha England akichezea timu zenye umri mkubwa kuliko yeye, ambapo
aliitwa kwenye timu ya U16 akiwa na miaka 14, na baadaye kwenye timu ya U17
akiwa na miaka 15.
Mwaka
2011 alipata mtoto wa kiume, aitwaye Archie Jack Wilshere.
TANK
Mwanamuziki wa Marekani, mzaliwa wa Wisconsin tarehe kama ya leo mwaka
1976 leo ametimiza miaka 39. Mwimbaji huyu na mtayarishaji wa muziki wa R&B
amepata kuwania Tuzo za Grammy na ametoa albamu nyingi ikiwemo
Now or Never. Pia ametoa single kama "Emergency" na "Sex
Music."
Kabla
ya kuingia kwenye muziki alikuwa mchezaji wa kandanda la Kimarekani na alipata
ofa nyingi za kucheza kwenye timu za vyuo lakini akazitosa na kuingia kwenye
muziki. Alitoa albamu ya Sex, Love, & Pain, ambayo
iliingia kuwania Tuzo za Grammy katika Albamu Bora ya R&B mwaka 2008.
Watoto
wake ni
Jordan, Ryen, Zoey, na Durrell Jr. Alirekodi wimbo
wa "Take My Time" akishirikiana na Chris Brown.
SOPHIE OKONEDO
Mwigizaji wa filamu aliyezaliwa
nchini Uingereza mwaka 1968. Alipata umaarufu mkubwa kutokana na
ushiriki wake katika filamu ya Hotel Rwanda mwaka 2005
na The Secret Lives of Bees mwaka 2008. Ushiriki wake katika filamu ya Tsunami:
The Aftermath ulimfanya ateuliwe kuwania Tuzo za Golden Globe. Alisoma katika Chuo
cha Sanaa za Maigizo cha Royal Academy kabla ya kupata
fursa ya kuingiza vipindi vya televisheni kwenye kituo cha BBC. Aliteuliwa
kuwania Tuzo za Academy kwa ushiriki wake kwenye filamu ya Hotel Rwanda.
Ana binti
mmoja, Aoife, aliyezaa na mpenzi wake wa zamani Eoin
Martin. Aliigiza kama May Boatwright akishirikiana
na Queen Latifah katika filamu ya mwaka
2008, The Secret Life of Bees.
J. EDGAR HOOVER
Mkurugenzi huyu wa zamani na wa kwanza wa Shirika la Upelelezi la
Marekani (FBI) alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1895 na akafariki Mei 2, 1972
akiwa na miaka 77. Alikuwa Mkurugenzi wa FBI kati ya mwaka 1935
hadi 1972 na ndiye mkurugenzi wa shirika hilo aliyekaa kwa miaka mingi zaidi
(37). Yeye ndiye aliyeanzisha utaratibu wa kumbukumbu za alama za vidole na na
maabara za uchunguzi (forensic laboratories).
Alikuwa
mwimbaji mzuri wa kwaya ya shule, mshiriki wa timu ya midahalo, ofisa wa akiba
wa jeshi tangu akiwa shule ya sekondari. Alitumia
FBI kuwatisha wanasiasa na wanaharakati na kutoa mafaili ya siri kwa wanasiasa. Huyu ndiye aliyemsaliti Martin Luther King Jr. kwa sababu
aliamini kwamba mwanaharakati huyo alikuwa anahatarisha usalama wa Marekani.
Baba
yake mkubwa alikuwa balozi wa heshima wa Uswisi nchini Marekani. Alikuwa
Mkurugenzi wa Kwanza wa FBI akiwa chini ya Rais Franklin D. Roosevelt na kumalizia chini ya
Rais Richard Nixon.
DIAMOND WHITE
Mwanamuziki huyu aliyezaliwa tarehe kama ya leo huko California,
Marekani mwaka 1999 anatimiza miaka 20. Ni maarufu katika muziki wa R&B na
pop na alimaliza akiwa wa tano katika awamu ya pili ya kipindi cha "The
X-Factor".
Alichaguliwa
katika utengenezaji wa kipindi cha "The Color
Purple" tangu akiwa na miaka nane na alishiriki kwenye ziara ya taifa.
Sauti yake ilitumika katika vipindi vya "Transformers:
Rescue Bots" na "Phineas and Ferb" kupitia Chaneli ya Disney.
Yeye na
mama yake walihangaika kiuchumi wakati alipokuwa anaanza maisha ya muziki,
wakati mwingine akilala kwenye kochi kwenye kibanda tu. Wakati akiwa katika
kipindi cha "The X Factor" alikuwa chini ya
uangalizi wa Britney Spears.
No comments:
Post a Comment