Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 23 May 2015

WANAUME CHANZO CHA WAJAWAZITO KUCHELEWA KLINIKI


Na Hastin Liumba, Nzega
KUCHELEWA kwa kina mama wajawazito na waliojifungua kuhudhuria Kliniki kunasababishwa na mfumo dume unaosababishwa na waume ama wenza wao, imeelezwa.

Hayo yalielezwa na mhudumu wa mama na mtoto wa kituo ha afya Bukene wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Kapufi alisema hayo baada ya ujumbe ulioongozwa na Afisa Habari na mawasiliano Anna Sawaki wa shirika lisilo la kiserikali la EGPAF linalopata ufadhili toka kwa mashirika ya USAID na CDC kutaka kufahamu hali halisi ya maudhurio ya wajawazito kliniki.

Alisema bado ipo haja kwa elimu kutolewa kwa wanaume juu ya umuhimu wa wajawazito na kina mama waliojifungua kuhudhuri kliniki kwa awamu zote nne kama ilivyo katika miongozo.

Alisema pamoja na mwitikio kuendelea kuwa mzuri bado wanaume wamekuwa kikwazo kwa wajawazito kuhudhuria kliniki na pengine kwa na imani potofu.

Alifafanua kuwa hali hiyo mara kadhaa imesababisha wajawazito kujifungulia majumbani hali ambayo ni hatari kwa afya ya mama na mtoto anayezaliwa.

Alisema kwa sasa kwa siku za kliniki kina mama wajawazito na waliojifungua kwa siku jumla ya kina mama 50 hadi 78 huhudhuria idadi ambayo nindogo.

Kuhusu wajawazito waliopimwa afya zao katika kipindi cha mwezi Januari hadi Aprili 2015 jumla walikuwa 588 kati yao 10 walikutwa na maambukizi ya VVU ambapo 7 kati yao wameanza tiba huku watatu wakikaa majibu na kuacha kuhudhuria kliniki.

Akizungumzia changamoto za kituo hiho mtoa huduma ya matunzo na tiba kwa wagonjwa wenye VVU Gramaliel Chimpaje alisema kituo kinakabiliwa na upungufu wa dawa za malaria za SP kwa wajawazito.

Alisema kwa mwaka 2014 dawa hizo hazikuja kabisa ambapo kwa mwaka 2015 ni SP 100 tu ndizo walizopokea na hadi sasa zimekwisha.

Alitaja changamoto nyingine ni wajawazito wanakutwa na maambukizi huacha kuhudhuria kliniki na hutoa vitisho kwa watoa huduma kutokanyaga majumbani mwao.

Aidha aliongeza kingine ni wajawazito wengi kuhudhuria kliniki wakiwa wamechelewa huku wengine huja wakiwa wamebakiza mwezi mmoja ama mitatu kujifungua.

Grace Leonard mama aliyejifungua alitoa wito kwa wajawazito na waliojifungua kuhudhuria kliniki mapema ili waweze kutambua afya zao na mtoto na akabainisha lugha za ukali kwa watoa huduma bado ni tatizo kwa wajawazito.

No comments:

Post a Comment