Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 29 May 2015

VIJANA 85 WENYE ITIKADI KALI WAJISALIMISHA KENYA

Serikali ilitoa msamaha kwa wale wote waliojiunga na Al Shabab baada ya kuuawa kwa wanafunzi 150 mjini Garissa
Takriban vijana 85 waliokuwa wamepokea mafunzo yenye itikadi kali wamejisalimisha kwa polisi nchini Kenya.

Vijana hao wamejisalimisha kwa serikali ya Kenya, ili kupokea msamaha uliotelewa kwa wale wote ambao wamepokea mafunzo ya itikadi kali ya kiislamu na kujiunga na kundi la wapiganaji wa Al-Shaabab.
Msemaji wa Serikali imesifu hatua ya vijana hao, akitaja kuwa itachangia pakubwa ukusanyaji wa taarifa za kijasusi.
Vijana 85 waliopokea mafunzo yenye itikadi kali wajisalimisha kwa serikali ya Kenya
Awali vijana hao walihofia kujisalimisha kwa hofu kuwa wangetengwa katika jamii na hata kufungwa gerezani.
Maafisa katika wizara ya mambo ya ndani wamesema kuwa vijana hao walikuwa kati ya umri wa mika ishirini na thelathini.
Serikali ya Kenya iliahidi kuwasamehe vijana hao mapema mwezi uliopita, kufuatia uvamizi katika chuo kikuu cha Garissa, ambapo zaidi ya watu 150 waliuawa.
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabaab walikiri kutekeleza shambulizi hilo ambalo limepelekea chuo hicgo kufungwa.
Al Shabaab inaitaka Majeshi ya Kenya yaondolewe Somalia
Kujasalimisha kwa vijana hao kumepiga jeki juhudi za serikali ya Kenya dhidi ya mafunzo ya itikadi kali, yanayochangia hatua ya vijana hao kujiunga na makundi ya kivita kama vile Al Shabab.
Kundi hilo kutoka Somalia linaaminika kuwa na wafuasi nchini Kenya ambapo limetekeleza mashambulizi kadha katika jitihada ya kuilazimisha serikali ya Kenya kuondoa majeshi yake nchini Somalia.
Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika Amisom ambao wanaisaidia serikali dhaifu ya Somalia kupigana na waasi wa Al Shabaab.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment