Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 30 May 2015

SERIKALI YAKARIBISHA WAWEKEZAJI BINAFSI KWENYE SEKTA YA UCHUKUZI

uc1
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2015/2016 bungeni mjini Dodoma leo.

uc2
 Mbunge wa Kisarawe (CCM) Bw. Suleiman Jafo akichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya uchukuzi leo bungeni mjini Dodoma.
…………………………………………………………….
Na Fatma Salum – Maelezo, Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imesema inakaribisha wawekezaji binafsi kwenye miradi mbalimbali ili kuboresha sekta za uchukuzi na hali ya hewa hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. Charles Tizeba wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge zilizowasilishwa kwenye mjadala wa bajeti ya wizara hiyo leo bungeni mjini Dodoma.
“Serikali inawakaribisha wawekezaji binafsi kuwekeza kwenye miradi ya kuboresha miundombinu ya uchukuzi na hali ya hewa kwa kuwa Serikali peke yake haiwezi kukamilisha miradi yote bila ya ushirikiano na wengine”
Dkt. Tizeba alisema Serikali ina mipango madhubuti ya kuboresha miundombinu nchini ikiwemo reli, bandari na barabara na kupitia dhana ya ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi (Public Private Partnership) itaweza kufanikisha mipango hiyo kwa ufanisi na kwa wakati.
Aidha Dkt. Tizeba aliongeza kuwa kupitia juhudi za Serikali baadhi ya miradi ipo katika hatua za awali ikiwemo uboreshaji wa viwanja vya ndege 11 kwenye mikoa mbalimbali nchini ambapo wataalamu wameshafanya upembuzi yakinifu (Feasibility Study) na fedha zikipatikana vitafanyiwa matengenezo mara moja.
Akizungumzia upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam Dkt. Tizeba alibainisha kuwa taratibu za kumpata mzabuni zinaendelea na akipatikana ujenzi wa gati namba 13 na 14 za bandari hiyo utaanza.
Leo Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta aliwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2015/2016 ambapo bunge lilikubali kupitisha zaidi ya shilingi bilioni 452.9.

No comments:

Post a Comment