Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 31 May 2015

MWANAMFALME WA UINGEREZA AIKASHFU FIFA


Mwana wa mfalme wa Uingereza, Prince William ametoa wito kwa shirikisho la soka duniani FIFA kuweka maslahi ya soka mbele ya matamanio ya kibinafsi.

Kwenye hotuba yake kabla ya fainali ya kombe la FA nchini Uingereza, William ambaye pia ni rais wa shirikisho la soka la FA nchini Uingereza.
ameilinganisha sakata ya FIFA na ile ya jiji la Salt Lake ilifyofanyika wakati Marekani ilikuwa inasaka tiketi ya kuandaa mashindano ya olimpiki ya barafu mnamo mwaka wa 2002 na kuilazimu kamati ya kimataifa ya Olimpiki kuimarika.
Blatter ametawazwa rais wa FIFA kwa muhula wa 5
"Inaonekana kuna mgawanyiko mkubwa kati ya wanaocheza na kushabikia mchezo huo na madai ya ufisadi yanayowakabili wasimamizi wa mchezo huo. Alisema"
"Matukio ya Zurich wiki hii yanasadifiana na wakati wa Salt Lake ambapo kamati ya Olimpiki, IOC ilipitia hali kama hii ya FIFA.
''Sawa na IOC inastahili kuonyesha ina uwezo wa kujali maslahi ya mchezo huo".
Gill asusia wadhfa katika FIFA
Wakati huo huo, Mamlaka ya Uswizi, imeanzisha uchunguzi zaidi kuhusu utoaji wa ruhusa ya uwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia mwaka wa 2018 na 2022 kwa mataifa ya Urusi na Qatar mtawalia.
Mwanamfalme William ndiye aliyeiongoza kamati ya Uingereza ya kuwania uwenyeji wa kombe la dunia la 2018 akiwa pamoja na mchezaji wa zamani wa Uingereza, David Beckham.
"wanaounga mkono FIFA wakiwemo wadhamini na mashirika ya jumuiya, wanastahili kuchukua jukumu la ya kushinikiza mabadiliko ndani ya FIFA.
Shirikisho la soka barani ulaya UEFA inapanga kuwa na mkutano kujadili iwapo watashiriki katika kombe la dunia Urusi au la
''Iwapo hatutafanya hivyo, tutakuwa hatuwatendei haki wapenzi wa mchezo huo na mchezo wasoka kwa jumla".
Kando na hayo, Mwenyekiti wa FA, Greg Dyke, amesema kuwa Uingereza iko tayari kuunga mkono hatua ya shirikisho la soka barani ulaya UEFA kususia kombe la dunia la 2018.
Wasimazizi wa soka barani Uropa wanapanga kukutana jijini Berlin wiki ijayo kufanya maamuzi ya iwapo watasusia mchuano wa kombe la dunia la mwaka wa 2018 utakaoandaliwa Urusi au la.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment