Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 29 May 2015

MYANMAR YAWAOKOA WAHAMIAJI 700

Myanmar haiwatambui watu wa jamii ya Rohingya kama raia wake
Myanmar imesema kuwa jwanamaji wake wamewaokoa takriban wahamiaji 700 waliokuwa wametelekezwa baharini na walanguzi wa bianadamu.

Msemaji wa serikali anasema kuwakundi hilo lilikuwa na wanawake na watoto 120.
Awali maafisa wa mataifa yaliyoko kwenye ukanda huo yalikutana kukubaliana kulipea swala hilo kipao mbele ilikuzuia maafa zaidi baharini.
Hata hivyo maafisa kutoka Myanmar na Umoja wa matafa walikabiliana vikali dhidi ya tuhuma za dhulma dhidi ya watu wa jamii ndogo ya Rohingya.
Myanmar yawaokoa wahamiaji 700
Naibu kamishena mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR, Volker Turk, aliuambia mkutano unaoendelea wa mzozo wa wahamiaji wa bara Asia, kuwa Myanmar inatakikana kuajibikia raia wote wa Nnchi hiyo bila ya kuwabagua wengine.
Taifa hilo haliwatambui watu wa jamii ya Rohingya kama raia wake.
Lakini mjumbe mmoja wa Myanmar Htin Linn, amesema kwamba taifa hilo halipaswi kulaumiwa pekee, ilihali swala zima la ulanguzi wa binadamu ndilo tatizo kuu kwa sasa.
Katika miezi michache iliyopita, maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakimiminika katika pwani ya Indonesia, Malaysia na Thailand huku mamia ya wengine wakiwa bado wamekwama baharini.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment