Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 29 May 2015

UYUI WARIDHIA KUGAWA JIMBO LA TABORA KASKAZINI


Na Hastin Liumba, UyuiBARAZAla madiwani wilaya ya Tabora (Uyui)mkoani Tabora kwa kauli moja wameridhia na kupendekeza kugawa halmashauri ya wilaya ya Tabora na jimbo la Tabora Kaskazini ili lipatikane jimbo la Ilolangulu.

Maamuzi hayo yalifikiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichoketi makao makuu ya wiloaya hiyo Isikizya.

Wakijadili kwenye baraza hilo madiwani hao walisema wameridhia kwa kauli moja jimbo hilo ligawanywe.

Walisema na kupendekeza kuwa jimbo jipya libaki na kata zote tisa zinazounda tarafa ya Ilolangulu.

Walisema kata hizo ni Ilolangulu, Mabama, Ibiri, Usagali, Ndono, Ufuluma, Isila, Makazi na Kalola.

Aidha walisema jimbo mama la Tabora Kaskazini liundwe na kata zote tisa ambazo ni Shitage, Bukumbi, Upuge, Ikongolo, Magiri Nsimbo, Isikizya, Igulungu na Ibelamilundi.

Walisema mapendekezo hayo yanatokana na ukweli kuwa jimbo la Tabora kaskazini kijiografia limetawanyika kiasi mbunge wake kushindwa kuwafikia wapiga kura wake.

Aidha kikao kililiridhi mkurgenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kitayarishe ramani na kuiwakilisha kwenye kikao cha kamati ya ushauri mkoa (RCC).

Aidha baraza hilo pia limeridhia na kupendekeza halmashauri ya hiyo igawanywe na kupatikana halmashauri ya wilaya ya Igalula.

Wakijadili madiwani hao walieleza halmashauri mama ya Tabora iendelezwe kama ilivyo sasa na kubaki na kata zote 18 inayounda tarafa za Ilolangulu na Uyui.

No comments:

Post a Comment