Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 29 May 2015

USHIRIKINA WATEKETEZA WATU 2,936

Jaji mstaafu, Amir Manento.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa ripoti kuhusu haki za binadamu nchini ya mwaka 2014 ikionyesha kuongezeka kwa matukio kadhaa ya uvunjaji wa haki hizo nchini vikiwamo vifo vya watu vinavyotokana na imani za ushirikina. Pia ripoti hiyo imeonyesha kuwa demokrasia nchini bado ni safari ndefu.

 
Ripoti hiyo iliyowasilishwa jana ilibainisha kuwa kwa matukio ya vifo vinavyotokana na imani za ushirikina yameongezeka mwaka 2010 hadi 2014 kutoka watu 2,583 hadi  2,936.   Aidha, ripoti hiyo inaonyesha kulitokea ajali za barabarani 21,791 ambazo zilisababisha vifo vya 3,437.
 
Ripoti ya LHRC iliyotolewa na Jaji mstaafu, Amir Manento, inasema kwamba ajali za barabarani zilitokea katika miji mikubwa.
Aidha, ripoti hiyo imesema watoto wa kike  1,302 walikeketwa katika kipindi cha mwaka 2014 katika mikoa ya Singida na Mara, huku wanawake 2,878 wakifanyiwa vitendo vya ubakaji wengi wao wakiwa ni watoto.
 
Ripoti hiyo ya LHRC ambayo hutolewa kila mwaka imesema mauji ya raia yanayofanywa na vyombo vya dola yamepungua kwa mwaka 2014.
 
Ripoti ya ukeketaji kwa mwaka 2009 ilionyesha kwamba wasichana 371 walibakwa wakati mauaji yaliyotokana na ushirikina yalikuwa 2,583.
 
Mauaji ya polisi katika Mkoa wa Pwani mwaka jana yametajwa katika ripoti hiyo kwamba yameleta madhara kwa kuwa chombo hicho ndicho kinacholinda amani hapa.
 
Kadhalika, Jaji  Manento alisema ikiwa miswada ya habari ya haki ya kupata taarifa na huduma za vyombo vya habari itasainiwa na Rais ili iwe sheria, itazika rasmi demokrasia nchini.
 
Jaji Manento alisema bado kuna safari ndefu kutekelezwa nchini ikiwamo kuminya uhuru wa kuwapo mgombea huru na rushwa kushamiri katika katika chaguzi, mambo yaliyopigiwa kelele na LHRC.
 
“Kutamka neno demokrasia na haki za binadamu bila kuzisimamia na kuzitekeleza, ni kazi bure,” alisema Jaji Manento wakati akiitangaza ripoti hiyo ya kila mwaka.
 
Ripoti hiyo ya mwaka 2014 ya LHRC inasema uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwishoni mwa jana, ulivurugwa kutokana na wasimamizi wa uchaguzi kuchelewa kufika vituoni na vurugu mbalimbali vituoni.
 
Alisema suala la demokrasia limekuwa likitamkwa mdomoni, lakini usimamizi na utekelezaji wake bado umeendelea kuwa mgumu.
 
Aidha, LHRC kimetabiri kwamba uchaguzi mkuu kwa mwaka huu utakuwa mgumu kwa sababu vyama vya upinzani vimeimarika na Chama Cha Mapinduzi (CCM), nacho kimejiimarisha.
 
Akizungumza kabla ya kuzindua ripoti hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo-Bisimba, aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), irekebisha dosari mbalimbali zilizojitokeza katika uandikishaji wa wapigakura kupitia mfumo wa BVR.
 
Aidha, Dk. Bisimba aliiomba serikali kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki mbalimbali zikiwamo za afya, elimu, kulindwa, kuwa huru kuchagua viongozi wa kisiasa, kushiriki katika siasa na kuachana na aina yoyote inayolenga kukandamiza haki za binadamu.
SOURCE: NIPASHE

No comments:

Post a Comment