Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 29 May 2015

UCHAGUZI WA FIFA 2015 UNAENDELEA HIVI SASA LICHA YA KASHFA YA RUSHWA

Blatter anakabiliana na mpinzani wake mkuu mwanamfalme Hussein kutoka Jordan
Wajumbe wa FIFA walioko nchini Uswizi wameanza kumpigia kura rais mpya wa shirikisho hilo la soka duniani huku shirikisho hilo likikabiliwa na shutuma za ufisadi.

Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter, ambaye ameongoza shirikisho hilo kwa miaka 17 amewataka wajumbe wa mkutano mkuu kuunga mkono nia yake ya kuchaguliwa tena kuongoza shirikisho hilo .
Akifungua mkutano mkuu wa FIFA mjini Zurich, Bwana Mr Blatter alibainisha kuwa shirikisho hilo linakabiliwa na matatizo - lakini akatoa wito kwa wajumbe kushughulikia matatizo hayo kwa pamoja
Lakini kabla upigaji kura , mpinzani mkuu wa bwana Blatter , Ali Bin al Hussein mwanamfale wa Jordan, aliwaomba wajumbe wa mkutano huo kumuunga mkono -- kwa ajili ya kuboresha mchezo wa soka
Siku ya pili ya Kongamano hilo ndio inayomchagua Rais wa FIFA.
Awali kumekuwa shinikizo kwa FIFA kuhairisha kongamano hili na pia uchaguzi wa urais.
hata hivyo maombi hayo yalifutiliwa mbali na inatarajiwa kuwa rais Sepp Blatter ataendelea mbele na uchaguzi ambao anakabiliana na mpinzani wake mkuu mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan.
Blatter amesema kuwa tuhuma zinazoenea sasa ni njama dhidi ya FIFA
Blatter alifungua kongamano hilo kwa kuomba kuweko na umoja miongoni mwa maafisa wa FIFA.
Amesema kuwa tuhuma hizo ni njama ya kuibua maswali dhidi ya uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2018 na 2022.
Blatter aliyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wajumbe, katika siku ya pili ya mkutano mkuu wa shirikisho hilo la kandanda duniani huko Zurich Uswisi.
Blatter ameahidi kukamilisha mabadiliko yatakayoirejeshea FIFA hadhi yake.
Blatter anakabiliana na mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan katika uchaguzi huo utakaofanyika leo.
Kwa upande wake mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan anasema kuwa yeye pekee yake ndiye aliye na nia ya kuleta mabadiliko ya kimsingi yatakayomaliza ufisadi na ulaji rushwa ndani ya FIFA.
Takriban wenyeviti wa mashirika 209 ya kandanda kote duniani wanakura moja kila mmoja .
Mwaandishi wa habari wa BBC, anasema kuwa Bwana Blatter anategemea uungwajji mkubwa kutoka kwa wajumbe wa mataifa ya Amerika, Afrika na Asia - ambao wanasema kuwa amefanya mengi katika kuboresha mchezo wa kandanda katika mataifa maskini.
FBI inachunguza uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2010
Naye Prince Ali anauungwaji mkubwa kutoka mataifa ya bara Ulaya.
Wajumbe hao wawili watahitaji zaidi ya robo tatu ya kura zote ili kupata ushindi wa moja kwa moja katika mkondo wa kwanza.
Hilo lisipofanyika, kutakuwa na mkondo wa pili wa upigaji kura, ambapo mshindi wa kura nyingi atatangazwa mshindi.
FIFA imekabiliwa wimbi la tuhuma za ufisadi ulaji rushwa na ubadhirifu mkubwa baada ya maafisa wake wakuu saba kukamatwa na polisi nchini Uswisi ilikujibu mashtaka nchini Marekani.
Maafisa wa kijasusi kutoka Marekani FBI wamependekeza kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa maafisa 14 wa FIFA kwa kula mlungula wa takriban dola shilingi 150 katika kipindi cha miaka 20.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment