Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 31 May 2015

UCHAGUZI MKUU BURUNDI WAFAA KUAHIRISHWA

Rais Nkurunzinza hakuhudhuria mkutano wa viongozi wa Afrika Mashariki
Kiti cha Rais Pierre Nkurunziza kikiwa wazi katika kikao cha Dar es Salaam leo hii.
Viongozi wa Afrika Mashariki wametoa wito kuwa uchaguzi wa Burundi uakhirishwe kwa angalau wiki sita na ghasia zimalizike.

Taarifa hiyo inafuatia mkutano wa viongozi wa Jumuia ya Afrika Mashariki mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Uamuzi wa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza kuania muhula wa tatu wa uongozi katika uchaguzi wa mwezi ujao, umesababisha maandamano kwa majuma kadha sasa.
Kiongozi wa Burundi hajakuwako kwenye mkutano huo.
Mara ya mwisho alipohudhuria mkutano kama huo awali mwezi May, maafisa wa jeshi walijaribu kumpindua.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment