Na Hastin Liumba, Tabora
MAHAKAMA ya mkoa wa Tabora imehukumu kifungo cha nje kwa kipindi cha mwaka moja Said Mlyome baada ya kupatikana na hatia ya kujifanya afisa mwandamizi wa usalama wa Taifa na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Akitoa hukumu hiyo jana hakimu wa mkazi wa mahakama ya mkoa wa Tabora, Bahati Chitepo alisema kwamba ameridhaka na ushaidi uliotolewa na upande wa mashitaka .
Alisema kwamba ameamua kutoa adhabu hiyo kwa mshitakiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia hovu kama aliyonayo mshitakiwa Said.
“Atakwenda kufanya kazi za kijamii kwa kipindi cha mwaka mmoja na kutofanya kosa la aima yoyote kwa kipindi hicho,“ alisema Chipeto.
Alisema kwa kosa hilo ambalo ndilo lilomtia hatiana mshitakiwa huyo kutumikia kifungo cha mwaka mmoja nje na kutofanya kosa lolote kwa kipindi hicho .
Chitepo alisema kutoka na kushindwa kuthibitisha kosa la pili la kujipita fedha kwa Ibrahimu John Mwakyusa kiasi cha sh 960,000 kwa ajili ya kuwatafutia kazi Benki ya kuu na Idara usalama wa Taifa.
Hakimu huyo alimuachia mtumiwa huyo kwa kosa hilo kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kudhibitisha kosa na hivyo kukabiliwa na kosa moja tu ma kutiwa hatiani kwa kifungo cha nje.
Awali mwendesha mashitaka wakili wa serikali, Ildephonce Mukandara aliambia mahakama hiyo kuwajulai 11 ,2013 Saidi Mlyomi alikamtwa na jeshi la polisi kwa kujifanya Afisa mwanandmizi kwa ajii ya kujipatia fedha kwa njia ya Udanganyifu.
Alisema kosa la pili kujipatia fedha kutoka kwa Ibrahimu John Mwakyusa kiasi cha sh 960.000 kwa ajili ya kumtafutia kazi idara ya Usalama wa Taifa ama Benki kuu Tanzania (BOT).
No comments:
Post a Comment