Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Wednesday, 28 January 2015
POLISI: HATUKUMPIGA RISASI PONDA
Na Hamida Shariff, Mwananchi
Morogoro. Shahidi wa pili katika kesi inayomkabili Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi, Morogoro kuwa, hawakuhusika kumpiga risasi mtuhumiwa huyo na kwamba alikamatwa katika Hospitali ya Muhimbili akitibiwa jeraha alilodai lilitokana na risasi.
RIPOTI YA WIZARA YAZIDI KUIWEKA PABAYA IMTU
Na Herieth Makwetta, Mwananchi
Dar es Salaam. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU) hakitafunguliwa mpaka pale upungufu ulioainishwa utakapofanyiwa kazi.
WANASAYANSI ‘BONGO’ KUSAFISHA MAJI YA KINYESI KUWA YA KUNYWA
Na Florence Majani, Mwananchi
Dar es salaam. Umeshikwa na kiu? Unaingia katika duka lililo jirani na kununua maji ya chupa kwa ajili ya kunywa. Lakini ukapatwa na udadisi kutaka kujua maji hayo yametengenezwa na nini. Unaposoma kilichotumika kutengeneza maji hayo, unagundua kuwa yametengenezwa kwa kinyesi.
BUNGE LAAHIRISHWA KUFUATIA KUKAMATWA KWA PROFESA LIPUMBA DAR
Kikao cha Pili cha Mkutano wa 18 wa Bunge la 10 kimeahirishwa muda huu mjini Dodoma baada ya Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, kuwasilisha hoja binafsi ya kutaka shughuli zote za serikali ziahirishwe mara moja ili kulishughulikia suala la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba.
NSSF, REAL MADRID KUZALISHA VIPAJI VYA SOKA TANZANIA
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau (aliyekaa kushoto) na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez (aliyekaa kulia) kwa pamoja wakisaini mkataba wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni wawakilishi kutoka pande hizo mbili. Kituo hicho kitakua na uwezo wa kupokea wanafunzi 108 kwa wakati mmoja. (Na Mpigapicha Wetu).
UNESCO YATAKA UBIA NA MWEDO
WASHINDI COPA COCA-COLA WAKABIDHIWA VITITA VYAO
Mabingwa wa Copa Coca-Cola 2014, timu ya Mkoa wa Dodoma
Washindi wa Copa Coca-Cola 2014 wamekabidhiwa zawadi zao za fedha kutoka kwa mdhamini wa michuano hiyo ya umri chini ya miaka 15 kwa wavulana na wasichana kampuni ya Coca-Cola. Fedha hizo kwa washindi mbalimbali tayari zimeingizwa kwenye akaunti zao.
KAMATI YATUPA RUFANI YA MWANZA KOMBE LA TAIFA WANAWAKE
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetupa rufani ya timu ya Mwanza kupinga uhalali wa wachezaji wawili wa Kigoma kwenye mechi yao ya robo fainali iliyochezwa jana (Januari 26 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
TAARIFA YA DRFA
Uongozi wa chama cha soka mkoa wa Dar es salaam (DRFA), umewaomba, mashabiki na wote wenye mapenzi mema ya kandanda, kujitokeza kwa wingi kuzishangilia timu za Dar es salaam zinazoshiriki ligi kuu,Daraja la Kwanza na michuano ya taifa Cup wanawake, ili kutoa hamasa kwa wachezaji.
Monday, 26 January 2015
WATOTO WA HOSNI MUBARAK WAACHILIWA HURU
Wana wawili wa aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak wameachiliwa kutoka jela, miaka minne baada ya kukamatwa na kuzuiliwa kwa pamoja na baba yao.
ASILIMIA MOJA YA MATAJIRI KUMILIKI IDADI YA WATU WOTE DUNIANI
Bill Gates na Warren Buffet
Huku wafanyibiashara na wanasiasa wa ngazi za juu wakikutana katika mkutano wa kiuchumi duniani mjini Davos wiki hii ,hisia tofauti zimetolewa kuhusiana na kuwepo kwa ukosefu wa usawa duniani bila kuisahau asilimia moja ya watu Matajiri duniani.
WATANZANIA WALILIA TAIFA HURU
Na Hastin Liumba, TaboraWAKATI Taifa likikiwa limetimiza miaka 54 tangu lipate uhuru wake kutoka kwa wakoloni sasa watanzania waanza kulilia uhuru Mpya kutokana na Udhalimu unaolikabilii taifa hili kwa sasa.
MAMA AUA WANAWE WAWILI TABORA
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu
Na Hastin Liumba, TaboraJESHI la Polisi mkoani Tabora linamshikiria mama mmoja mkazi wa kata ya Chemchem katika Manispaa ya Tabora Zuhura Masudi 25 kwa kosa la kuwanyonga hadi kufa watoto wake wawili.WABUNGE WABEBA KASHFA YA NBC
Na Mwandishi Wetu
KASHFA ya kuuzwa kwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa bei ya
kutupwa inayotarajiwa kuwasilishwa katika Mkutano wa 18 wa Bunge unaoanza kesho Mjini Dodoma, inatajwa kuwa moja ya ajenda ambazo zitatawala mwenendo wa
mjadala wa vikao vya Bunge.
KAZI IMEKWISHA ESCROW!
Profesa Sospeter Muhongo akitangaza kujiuzulu wadhifa wake wa uwaziri wa Nishati na Madini Jumamosi, Januari 24, 2015
Na Sophia Yamola
KAZI imekwisha. Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter
Muhongo amejiuzulu, Baraza la Mawaziri nalo limebadilishwa.
TANZANIA KUHODHI LIGI YA MPIRA WA WAVU
Tanzania imechaguliwa tena kuwa wenyeji wa michuano ya mpira wa wavu ya mataifa ya Afrika (All Africa Games) itakayofanyika mapema mwezi wa nne mwaka huu.
BINTI WA KIDOSI ALIYEOLEWA NA 'MSWAHILI' YAMEMKUTA!
Sarika na mume wake Timothy wameachana baada ya Sarika kudai kwamba mume wake amekuwa akimdhulumu
Je unakumbuka kisa cha wapenzi wawili waliozua gumzo nchini Kenya?
MTAWA AMTUKANA MJUMBE WA UMOJA WA MATAIFA
Kiongozi Kibudha, Ashin Wirathu, aliyetoa matusi makali kwa mjumbe wa UN
Umoja wa Mataifa umewataka wanasiasa na viongozi wa kidini Nchini Myanmar kulaani matamshi ya uchochezi na chuki yaliyotolewa na kiongozi mmoja wa Kibudha dhidi ya mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa.
WANAUME HURU KUJISAIDIA WAKIWA WAMESIMAMA
Mahakama moja nchini Ujerumani imempa idhini mwanamume mmoja kujisaidia haja nodgo akiwa amesimama baada ya mwenye nyumba kutaka alipwe akidai kuwa sakafu ya bafu lake iliharibiwa na mkojo wa mpangaji wake.
KAMANDA WA LRA KUPANDISHWA KIZIMBANI ICC
Dominic Ogwen
Kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la waasi la Lord resistance Army, Dominic Ong'wen atafikishwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC mjini the hague nchini uholanzi. atakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita.
KASISI WA KWANZA MWANAMKE KUAPISHWA UINGEREZA
Libby Lane kuwa kasisi wa kwanza mwanamke
Kanisa moja nchini Uingereza hii leo litamuapisha mwanamke wa kwanza kuwa kasisi.
MSAFARA WA JESHI WASHAMBULIWA MALI
Ripoti kutoka nchini Mali zinasema kuwa watu wasiojulikana wameshambulia msafara wa kijeshi karibu na mji wa Timbuktu.
FDL KUSIMAMA KUPISHA VIPORO VYA POLISI MARA
Mechi za raundi ya 20, 21 na 22 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa makundi yote zimesimamishwa ili kupisha Polisi Mara imalize mechi zake za viporo, na timu zote zicheze mechi zao za raundi zilizobaki kwa pamoja.
MPANGO WA BRN SEKTA YA ELIMU UNA MAPUNGUFU - HAKIELIMU
Kaimu Mkurugenzi wa HakiElimu, Godfrey Boniventura (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Wengine kushoto na kulia ni maofisa wa taasisi ya HakiElimu wakiwa katika mkutano huo.
TIMU YA ARSENAL YAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI YA TTCL
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Dam Stone (kulia) akipokea zawadi kutoka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) iliyokabidhiwa na Meneja wa Masoko na Usambazaji wa TTCL, Robert Noel kabla ya kuanza mazungumzo ya kibiashara kati ya pande hizo mbili.
Monday, 19 January 2015
WARIOBA ATAJWA URAIS KUPITIA UKAWA
Na
Mwandishi Wetu
UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) inadaiwa kuwa
unakusudia kumsimamisha Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba kuwania urais mwaka
huu dhidi ya wagombea wa vyama vingine, kikiwemo Chama cha Mapinduzi (CCM).
ARSENAL YAWASHANGAZA MABINGWA WA EPL
Santi Carzola alifunga bao moja na kutengeza jengine na kuisadia Arsenal kuicharaza Man City mabao 2-0 nyumbani Manchester.
MAVAZI YA MHUBIRI YAWAACHA VINYWA WAZI
Mhubiri mmoja nchini Iran amewaacha watu vinywa wazi kwa kuvalia vazi la rangi ya manjano.
DUBAI YAONGOZA KWA UAMINIFU
Dubai imejinyakulia sifa ya kipekee katika kupima Imani za jamii kwa pochi iliyoangushwa mtaani,na ikarejeshwa kwa mhusika mara moja.
UPINZANI CONGO DR WASEMA, KATIBA IMEPINDULIWA
Wabunge wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wamekubali mswada ambao wadadisi wanasema unakusudiwa kumpa Rais Joseph Kabila idhini ya kubaki madarakani, baada muhula wake wa pili kumalizika.
MALI HAINA WAGONJWA WAPYA WA EBOLA
Waziri wa Afya wa Mali amesema nchi hiyo kwa sasa haina maambukizi ya virusi vya Ebola baada ya siku 42 za kutokuwa na wagonjwa wapya walioambukizwa virusi vya ugonjwa huo.
BOKO HARAM WAFANYA UVAMIZI CAMEROON
Askari jeshi wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa kundi haramu Boko Haram wameteka watu zaidi ya 60 katika nchi jirani ya Cameroon imethibitika.
SERIKALI YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO KUTOKA KWA SERIKALI YA CHINA
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akibadilishana hati ya makabidhiano ya vifaa vya michezo na Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing (kulia) wakati wa hafla ya kukabibidhiana vifaa hivyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Shija)
WAZIRI MUKANGARA AZINDUA MFUMO WA KUNUNUA FILAMU KWA NJIA YA MTANDAO
Dk. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Na Benjamin Sawe, WHVUM
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara amewasihi wadau wa filamu kuongeza ujuzi na kubadilika ili kuendana na mabadiliko yanayotokea ulimwenguni katika masuala yanayohusu tasnia hiyo hasa katika suala zima la teknolojia ya uandaaji na usambazaji wa filamu.
Friday, 16 January 2015
KASHFA NZITO YAIBUKA BANDARI
Na Fidelis Butahe, Mwananchi
Dar es Salaam. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeitaka menejimenti ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kurejesha nyongeza ya fedha zote za malipo ya safari ilizowalipa watendaji wake tangu mwaka 2011, baada ya kubainika kuwa zililipwa bila kuidhinishwa na Msajili wa Hazina.
COASTAL UNION WAICHIMBA MKWARA POLISI MORO
Kikosi cha Coastal Union
NA MWANDISHI WETU, TANGATIMU ya Coastal Union imeitahadharisha timu ya Maafande wa Polisi Morogoro kwa kuiambia isitarajie kuwa itaweza kuchukua pointi tatu muhimu wenye kwenye mechi yao ya Ligi kuu itakayochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani badala yake wajiandae kupokea kipigo kutoka kwa timu hiyo kutokana na maandalizi kabambe waliyoyafanya kuelekea mechi hiyo.
UKAWA WAANZA SAFARI YA URAIS
Na Kelvin Matandiko, Mwananchi
Dar es Salaam. Wakati CCM ikisubiri Februari kufanya tathmini kuona kama baadhi ya wagombea wake wa urais wametekeleza masharti ya adhabu zao, washindani wao wa Ukawa, Jumanne ijayo watakutana kujadili mambo mbalimbali, ukiwamo mchakato wa kuwapata wagombea wake wa urais, ubunge na udiwani, imefahamika.
HUDUMA YA KUOKOA WATUMISHI WA UMMA KENYA
Serikali ya Kenya imeanzisha mpango kabambe wa kutoa huduma za kuokoa kwa kutumia ndege na magari kwa watumishi wa umma nchini humo.
Huduma hiyo imezinduliwa kwa ushirikiano na shirika la bima ya afya,shirika la msalaba mwekundu na kundi lamadaktari wanaosafiri kwa ndege la AMREF.
Kenya inakuwa nchi ya pili baada ya Afrika Kusini kutoa huduma ya aina hii.
Victor Kenani alkuwepo kwenye uzinduzi wa mpango huo ambapo Rais Uhuru Kenyatta alihudhuria
CREDIT: BBC
KESI YA RITA JEPTOO YAANZA KUSIKILIZWA
Mwanariadha Rita Jeptoo
Kesi ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu ya bingwa mara tatu wa Boston Marathon Rita Jeptoo wa Kenya imeanza leo hii mjini Nairobi lakini chama cha riadha kimesema hakitatangaza hukumu ya Jeptoo hadi wiki ijayo.
RONALDO DE LIMA KUREJEA UWANJANI
Ronaldo de Lima alivyo sasa
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya brazil Ronaldo Luís Nazário de Lima anatarajia kurejea tena dimbani.
HATARI: TAZAMA UREMBO BANDIA ULIVYOTAKA KUMPA MAUTI BINTI HUYU!
Baada ya masaibu ya kujitakia urembo bandia, Urach hawezi tena kutembea kwani kwa sasa anatumia kiti cha magurudumu
Mwanamke aliyemaliza katika nafasi ya pili ya mashindano ya urembo amesema kupenda sana kujiweka urembo bandia nusura umletee mauti yake.
OLE WENU MSIOPENDA MAZOEZI
Je ulijua kama watu wengi barani Ulaya wanakufa kwa kukosa kufanya mazoezi ikilinganishwa na idadi ya watu wanaokufa kutokana na ugonjwa wa kisukari?
HEZBOLLAH YASEMA, ISRAEL INATUPELELEZA
Wapiganaji wa kuni la Hezbollah
Kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Kilebanoni la Hezbollah amethibitisha taarifa zinazodai kuwepo mmoja wa viongozi wa juu ndani ya kundi hilo anatuhumiwa kutumwa na Israel kuwapepeleza.
GUINEA KUTOKOMEZA EBOLA KWA SIKU 60
Mila na tamaduni za Watu zimesababisha Watu wengi kupoteza maisha kutokana na Ebola
Mipango ya mamlaka za afya nchini Guinea ni kuutokomeza ugonjwa wa Ebola kwa siku sitini. Mpango huu unategemea kuhamasishwa kwa Watu katika maeneo yote yaliyoathiriwa nchini Guinea kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
UBELGIJI YAFANYA MSAKO MKALI WA MAGAIDI
Polisi wa Ubelgiji
Ubelgiji imefanya operesheni kali ya ugaidi ikiwasaka watuhumiwa wanaodaiwa ni wapigani wa Kiislamu waliorejea kutoka Syria.
Subscribe to:
Posts (Atom)