Mashabiki wanne wa kilabu ya Chelsea walioshtumiwa kwa kukataa kumrusu mtu mmoja mweusi kuingia katika treni ya Paris Metro wamepigwa marufuku kuhudhuria mechi mechi za soka kwa takriban miaka mitano.
Richard Barklie,kutoka Carrickfergus,Northern Ireland na Joshua Parsons pamoja na William Simpson wote kutoka Surrey walipigwa marufuku kwa miaka mitano katika mahakama ya Stratford.
Jordan Munday ,kutoka eneo la Sidcup Kent,alipigwa marufuku ya miaka mitatu.
Waliagizwa kwamba hawawezi kuhudhuria mechi nyumbani ama ugenini.
Jaji wa wilaya Gareth Branston alisema kwamba chuki ya kibaguzi ilionyeshwa na mashabiki wa Chelsea katika treni hiyo ya Paris.
Aliaambia mahakama hiyo kwamba kisa hicho kiliharibu sifa ya soka ya Uingereza barani Ulaya.
Ghasia zilizuka wakati mashabiki wa Chelsea walipokuwa katika mji huo wa Ufaransa ili kushabikia mechi ya vilabu bingwa Ulaya kati ya Chelsea na Pasris Saint Germain tarehe 17 februari.
Baadaye kanda ya video iliibuka ikimuonyesha raia mmoja wa Ufaransa Souleymane Sylla akisukumwa nje ya treni huku kukiwa na wito wa ''sisi ni wabuguzi na hivyo ndivyo tunavyopenda''.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment