Amisi Tambwe wa Yanga akifanyiwa madhambi na mchezaji wa Gor Mahia katika mechi ya ufunguzi Julai 18, 2015.
Na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com
YANGA, Gor Mahia ya
Kenya, Limbe Leaf Wanderers ya Malawi na Al Hilal ya Sudan ndizo timu pekee ambazo
zina historia ya kususia mechi wakati mashindano ya Kombe la Kagame yakiwa
yanaendelea.
Kwa nyakati tofauti,
timu zimepata kususia mechi zao kwa sababu mbalimbali, ingawa ni Yanga pekee
ambayo ilipata kuadhibiwa vikali kwa kufungiwa kushiriki kwa miaka mitatu mwaka
2008.
Yanga ilikuwa
imesusia mechi yake ya kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Simba mwaka 2008,
lakini Limbe Leaf ilisusia mwaka 1981, Gor Mahia iligomea mchezo mwaka 1982 na
Al Hilal ilisusia mwaka 1994.
Ifuatayo ni
kumbukumbu sahihi ya ripoti za mashindano hayo ambazo zinaonyesha namna timu
hizo tatu zilivyopata kususia mechi zao:
Mwaka 1981 – Limbe Leaf yagomea penati ya
Simba
Mashindano ya
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kwa mwaka 1981 yalifanyika katika miji ya
Nairobi na Kisumu nchini Kenya kati ya Januari 18 na Februari Mosi.
Jumla ya timu
saba zilishiriki mashindano hayo ambazo ni Limble Leaf Wanderers (Malawi),
Kabwe Warriors (Zambia) na AFC Leopards (Kenya) ambazo zilikuwa Kundi A. Kundi
B lilikuwa na KMKM (Zanzibar), Simba SC (Tanzania), Nile Breweries (Uganda) na
Gor Mahia (Kenya).
Mwaka 1981 Simba
iliingia fainali na bao 1 na ilimaliza mashindano hayo ikiwa na bao hilo hilo
moja.
Katika michuano
ya awali Simba SC ilipangwa Kundi B mjini Kisumu, na iliifunga Nile Breweries
ya Uganda 1-0 Januari 18, halafu ikatoka suluhu na KMKM ya Zanzibar na Gor
Mahia ya Kenya.
Gor Mahia yenyewe
ilianza kwa kuichapa KMKM mabao 2-0, kipigo ilichokitoa pia kwa Nile Breweries,
hivyo ikakusanya pointi 5 na kuongoza kundi hilo. Simba ilishika nafasi ya pili
na kufuzu kwa nusu fainali.
Kwenye nusu
fainali Simba ilikutana na Limbe Leaf mjini Nairobi Januari 29, ambapo Limbe
Leaf ilijipatia bao moja na wakati ikiongoza kwa goli hilo katika dakika ya 86 mlinzi
wake akaunawa mpira kwenye eneo la hatari, Simba wakapata penati.
Hata hivyo,
wachezaji wa timu hiyo ya Malawi walitoka nje ya uwanja kugomea penati hiyo
waliyodai ilikuwa na utata. Jitihada za kuwashawishi warejee kuendelea na mechi
zikagonga mwamba.
Hivyo, katika
mkutano maalum Cecafa ikaamua kuipa ushindi Simba na kuipeleka katika fainali
ambako ilifungwa 1-0 na Gor Mahia. Bao hilo lilifungwa na Nashon Oluoch 'Lule'.
Gor Mahia katika
nusu fainali ilikuwa imeifunga Kabwe Warriors ya Zambia mabao 2-1 siku hiyo ya
Januari 29.
Limbe Leaf
Wanderers ilijifariji na nafasi ya mshindi wa tatu baada ya kuifunga Kabwe
Warriors mabao 2-0 Januari 31.
Matokeo kamili ya
mechi za mashindano hayo ni haya:
Kundi A
Limble Leaf W.
3-1 Kabwe Warriors
AFC Leopards 0-0 Limble Leaf Wanderers
Kabwe Warriors
3-1 AFC Leopards
1.Limble Leaf Wd. 2 1
1 0 3- 1
3 [Malawi]
2.Kabwe Warriors 2
1 0 1 4-
4 2
[Zambia]
3.AFC Leopards 2
0 1 1 1-
3 1
[Kenya]
Kundi B
KMKM 0-2 Gor Mahia
Simba SC 1-0 Breweries
Gor Mahia 2-0 Breweries
Simba SC 0-0 KMKM
Gor Mahia 0-0 Simba SC
Breweries 1-0 KMKM
1.Gor Mahia 3
2 1 0 4-
0 5
[Kenya]
2.Simba SC 3
1 2 0 1-
0 4
[Tanzania]
3.Breweries 3
1 0 2 1-
3 2
[Uganda]
4.KMKM 3
0 1 2 0-
3 1
[Zanzibar]
Nusu fainali
Limble Leaf W. vs
Simba SC [Jan 28; Simba ilipewa ushindi wa mabao 2-0; awali ilifungwa bao 1-0 lakini
Limbe Leaf Wanderers iligomea penati na hivyo Simba ikapewa ushindi]
Gor Mahia 2-1 Kabwe Warriors
Mshindi wa tatu
Limble Leaf W.
2-0 Kabwe Warriors
Fainali
Gor Mahia 1-0 Simba SC
Mwaka 1982- Gor yapomea penati dhidi ya
Leopards
Mwaka 1982 AFC
Leopards ilipambana na mahasimu wao Gor Mahia kwenye nusu fainali jijini
Nairobi wakati mashindano hayo yalipofanyika nchini Kenya. Hadi dakika 90
zinamalizika, matokeo yalikuwa suluhu, hivyo sheria ya penati tano tano ikabidi
itumike kumpaka mshindi.
Hata hivyo, Gor
Mahia iligomea sheria hiyo ikitaka uwepo muda wa nyongeza, lakini Cecafa
ikashikilia kwamba lazima matuta yatumike. Gor ikagoma, ikabidi AFC Leopards
ipewe ushindi wa mezani wamabao 2-0 na kusonga fainali ambako ilitawazwa kuwa
mabingwa baada ya kuichapa Rio Tinto ya Zimbabwe bao 1-0.
Mashindano ya
mwaka 1982, ambayo yalifanyika kuanzia Februari 13 hadi 25, yalishirikisha timu
nane zilizogawanywa katika makundi mawili ambapo Kundi A lilikuwa mjini Nairobi
likihusisha timu za AFC Leopards, Rio Tinto ya Zimbabwe, Ujamaa ya Zanzibar na
Information Club ya Somalia.
Kundi B lilikuwa
mjini Kisumu likihusisha timu za Gor Mahia, Bata Bullets, Yanga na Kampala City
Council.
Matokeo kamili ya
mashindano hayo ni kama ifuatavyo:
Kundi A [Nairobi]
13- 2 AFC
Leopards 2-0 Rio Tinto
14- 2 Ujamaa 1-0 Information Club
16- 2 Rio
Tinto 4-1 Ujamaa
17- 2 AFC
Leopards 2-0 Information Club
19- 2 Ujamaa 0-3 AFC Leopards
20- 2 Rio
Tinto 1-1 Information Club
1.AFC Leopards 3
3 0 0 7- 0
6
[Kenya]
2.Rio Tinto 3
1 1 1 5-
4 3
[Zimbabwe]
3.Ujamaa 3
1 0 2 3-
7 2
[Zanzibar]
4.Information C. 3
0 1 2 1-
4 1
[Somalia]
Kundi B [Kisumu]
13- 2 Gor
Mahia 1-1 Bata Bullets
14- 2 Young
Africans 2-1 Kampala City Council
16- 2 Gor
Mahia 1-0 Kampala City Council
17- 2 Young
Africans 1-0 Bata Bullets
19- 2 Gor
Mahia 3-1 Young Africans
20- 2 Bata
Bullets 2-0 Kampala City Council
1.Gor Mahia 3
2 1 0 5-
2 5
[Kenya]
2.Young Africans 3
2 0 1 4-
4 4
[Tanzania]
3.Bata Bullets 3
1 1 1 3-
2 3
[Malawi]
4.Kampala CC 3
0 0 3 1-
5 0
[Uganda]
Nusu fainali
22- 2 AFC
Leopards 2-0 Gor Mahia
23- 2 Rio
Tinto 2-1 Young Africans
Mshindi wa tatu
25- 2 Gor
Mahia 2-1 Young Africans
Fainali
25- 2 AFC
Leopards 1-0 Rio Tinto
Mwaka 1994 – Al Hilal yagoma kucheza na Merreikh
NIMEWAHI kuandika
huko nyuma kwamba hakuna michuano ya KLabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati
iliyokuwa na mizengwe na upendeleo wa wazi kama ya mwaka 1994. CECAFA ilifumbia
macho mambo maovu kabisa kwenye kandanda, ikiwabeba wenyeji kwa mbeleko ya
chuma hadi kufanikisha azma yao.
Kwanza kabisa Silver
Strikers ya Lilongwe, Malawi iliwasili siku chache kabla ya mashindano lakini
ilikataliwa na Katibu Mkuu wa CECAFA James Tirop wa Kenya kwa maelezo kwamba
ilichelewa kujiandikisha;
Gor Mahia ya
Kenya ilichelewa kuwasili katika mechi ya ufunguzi dhidi ya El Merreikh, lakini
haikuadhibiwa;
Kwa hiyo Silver
Strikers ilibakia mjini Khartoum kwa siku chache kwa matumaini ya kuruhusiwa
kushiriki bila mafanikio, hatimaye ikarejea kwao ikiwa imepoteza gharama nyingi.
Kutokana na hali
hiyo ya ubabashaji, Malawi ilijitoa CECAFA, ikifuatia hatua ya awali ya Zambia na
Zimbabwe, na hazikurejea tena, badala yake zikajiunga na Shirikisho la Soka
Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Michuano ya mwaka
1994 ilifanyika katika miji ya Khartoum na Port Sudan. Kundi A lililokuwa mjini
Khartoum lilizishirikisha timu za El-Merreikh (Sudan), Simba (Tanzania),
Express (Uganda) na Gor Mahia (Kenya).
Kundi B la mjini
Port Sudan lilikuwa na mabingwa watetezi, Yanga (Tanzania), El-Hilal Port
Sudan, Electric (Ethiopia) na Shangani (Zanzibar).
Michuano hiyo
iliyoanza Januari 8 na kumalizika Januari 20 iliingia dosari Januari 14 wakati
Simba, ikiwa inaongoza kwa mabao 2-1 dhidi ya El-Merreikh, ilizimiwa taa
uwanjani na wachezaji wake kupigwa na mashabiki, ambapo kiungo Nico Kiondo
alichomwa kisu.
Simba, ambayo
ilikuwa inaongoza katika kundi A, iliamua kujitoa mashindanoni na ilikuwa
inazishauri timu nyingine za Tanzania, Yanga na Shangani zijitoe. Hata hivyo,
timu hizo mbili hazikujitoa.
Kwa hali hiyo,
El-Merreikh iliyokuwa inashika nafasi ya pili kwenye kundi hilo, sasa
ilipangiwa kucheza na mshindi wa pili wa kundi B, El-Hilal. Lakini katika hatua
ya kushangaza, El-Hilal iligoma kucheza na El-Merreikh kwa madai kwamba hiyo
haikuwa timu ambayo ilipaswa kupambana nayo na hivyo Shangani iliyoshika nafasi
ya tatu kwenye kundi B ikapambana na El-Merreikh katika nusu fainali, ambapo
ilifungwa bao 1-0.
Yanga nayo
ilibidi ipambane na Express waliokuwa washindi wa tatu kwenye kundi A. Katika
mchezo wa nusu fainali, Yanga ilitolewa na timu hiyo ya Uganda kwa penati 5-4
baada ya kutoka sare ya bao 1-1 hadi muda wa ziada, hivyo ikawa imeutema
ubingwa huo iliouchukua nchini Uganda mwaka 1993. Katika kutafuta mshindi wa
tatu, Yanga iliifunga Shangani mabao 2-1.
El-Merreikh ndiyo
iliyotwaa ubingwa huo kwa kuifunga Express mabao 2-1 kwenye fainali.
Kwa kweli michuano
hiyo ilikuwa na dosari kubwa, kwani tangu awali ilionekana wazi kwamba Wasudani
walikuwa wanapendelewa na wala CECAFA haikuweza kuchukua hatua zozote za
tahadhari hata pale wachezaji wa Simba walipofanyiwa fujo.
Hebu tuangalie
namna mashindano hayo yalivyokwenda:
08/01/1994:-
Shangani 0 vs El-Hila 1
09/01/1994:-
Yanga 0 vs Electric 0
09/01/1994:- Simba
1 vs Express 2
09/01/1994:- El-Merreikh
1 vs Gor Mahia 1
11/01/1994:-
Shangani 2 vs Electric 1
11/01/1994:- Express
1 vs El-Merreikh 2
12/01/1994:-
Yanga 1 vs El-Hilal 1 (Fumo Felician/Amir Moussa)
12/01/1994:- Simba
1 vs Gor Mahia 0
14/01/1994:-
*Simba 2 vs El-Merreikh 1 (Ramadhani Lenny, Nteze John/?) - mchezo ulivunjika
dakika ya 88).
14/01/1994:- Yanga
2 vs Shangani 1
14/01/1994:- Express
1 vs Gor Mahia 0
14/01/1994:- El-Hilal
0 vs Electric 0
Kundi A
1.El Merreikh 3
2 1 0 3-
2 5
[Sudan]
2.Express FC 3
2 0 1 4-
3 4
[Uganda]
3.Simba SC 3
1 0 2 3-
2 2
[Tanzania]
4.Gor Mahia 3
0 1 2 1-
4 1
[Kenya]
[NB: bila mabao ambayo El Merreikh iliyopewa
dhidi ya Simba]
Kundi B
1.Young Africans 3
1 2 0 3-
1 4
[Tanzania]
2.El Hilal 3
1 2 0 2-
1 4
[Sudan]
3.Small Simba 3
1 0 2 2-
3 2
[Zanzibar]
4.Mebrat Hail 3
0 2 1 0-
2 2
[Ethiopia] [aka EELPA]
NUSU FAINALI:
17/01/1994:-
El-Merreikh 1 vs Shangani 0 (Zahir Abdulghani 90)
18/01/1994:-
Yanga 1 (4) vs Express 1 (5) (Constantine Kimanda 14, pen: Stephen Mussa,
Kenneth Mkapa, Tungaraza, Mohammed Hussein/ Robert Aloro 52, pen:)
MSHINDI WA TATU:
20/01/1994:-
Yanga 2 vs Shangani 1
FAINALI:
20/01/1994:-
El-Merreikh 2 vs Express 1 (Fattah Rahman Santo (mawili)/Issa Sekatawa).
[kadi nyekundu katika kipindi cha pili: Fatah
El Rahman Faraq (Merreikh) na Abdul Nsubuga (Express)]
Mwaka 2008 –
Yanga yagoma kucheza na Simba
KATIKA hali ya kushangaza, mwaka 2008 Yanga iligoma kupeleka
timu uwanjani kucheza na mahasimu wao Simba SC katika mechi ya kutafuta mshindi
wa tatu wa Kombe la Kagame jijini Dar es Salaam.
Hii ilikuwa mechi ya kwanza ya kimataifa kwa mojawapo ya
timu hizo kuigomea pindi zikitarajia kukutana uso kwa uso, ingawa huko nyuma
zilishawahi kukimbiana katika ligi na mashindano mengine ya ndani.
Kwa kawaida, timu hizi zinapokutana, mbali ya kutafuta
ushindi, lakini huangalia zaidi heshima kwani kupoteza humaanisha mambo mengi,
ikiwemo migogoro ya uongozi.
Sababu ambazo
Yanga ilizitoa zilikuwa ni pamoja na upendeleo wa Cecafa kwa Simba na ikadaiwa
kwamba kulikuwa na njama za kuhakikisha Yanga inafungwa mechi hiyo.
Mashindano ya
mwaka huo yalifanyika jijini Dar es Salaam kati ya Julai 12 na 27
yakishirikisha jumla ya timu 10 zilizogawanywa kwenye makundi matatu.
Tanzania
iliwakilishwa na timu mbili kwa vile ni mwenyeji, lakini Rwanda ilikuwa na
wawakilishi wawili kwani APR ilikuwa inatetea ubingwa wake.
Wawakilishi wa
Sudan waliondolewa, lakini timu za Société Immobilière de Djibouti – SID ya
Djibouti na Denden ya Eritrea zilijitoa mapema mwezi Julai kutokana na
kukabiliwa na ukata.
Kundi A lilikuwa mjini
Dar es Salaam na timu za Simba, Tusker FC ya Kenya, Vital’O ya Burundi na
Banaadir Telecom ya Somalia.
Kundi B lilikuwa
mjini Morogoro likiwa na timu za URA ya Uganda, Rayon Sport ya Rwanda na Awassa
Kenema ya Ethiopia; na Kundi C lilikuwa mjini Dar es Salaam likiwa na timu za
Yanga, APR na Miembeni ya Zanzibar
Simba iliongoza
Kundi A ambapo ilianza kwa kufungwa 3-2 na Tusker, Ikaiadhibu Banaadir Telecom
5-0 na kuichapa Vital’O 1-0.
Yanga nayo
iliongoza Kundi C baada ya kutoka sare ya 2-2 na APR na kuifunga Miembeni 1-0,
hivyo kuikwepa kiaina Simba katika robo fainali, kwani kama ingeshika nafasi ya
tatu ilibidi ipambane nayo.
Katika robo
fainali, Simba iliifunga APR mabao 2-0na Yanga ikaifunga Vital’O 2-0 na kutinga
nusu fainali. Wengi wakabashiri kwamba huenda timu hizo zingekutana fainali.
Lakini katika
nusu fainali, Julai 24 Simba ikafungwa 1-0 na URA baada ya mchezo kwenda hadi
dakika 120. Bao la Eric Obua la dakika ya 111 ndilo lililoiua Simba iliyokuwa
inanolewa na Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, ambayo siku hiyo iliwakilishwa na Amani
Simba, Nico Nyagawa, Ramadhan Wasoo, Kelvin Yondan, Henry Joseph, Anthony
Matangalu (Emeh Izechukwu), Mohamed Banka (Ulimboka Mwakingwe), Ramadhan
Chombo, Obinwa Orji (Adam Kingwande), Meshack Abel, Mussa Hassan
"Mgosi". Izechukwu aliikosesha penati katika dakika ya 119.
URA iliyokuwa
inafundishwa na Moses Basena, iliwakilishwa na Abbey Dhaira, Johnson Bagoole,
Manco Kaweesa, Joseph Owino, David Kyobe (Martin Muwanga), Ismael Kigozi, Mussa
Docca, Robert Okello (Jackson Ssenabulya), Dan Wagaluka, Henry Kiseka (Eric
Obua), Samuel Mubiru.
Yanga nayo Julai 25
ikatolewa na Tusker FC kwa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Simon Mburu kunako
dakika ya 53. Siku hiyo Yanga, ambayo ilikuwa inanolewa na Mserbia Dusan
Kondic, iliwakilishwa na Ivo Mapunda, Shadrack Msajigwa, Wisdom Ndhlovu, George
Owino, Nurdin Bakari, Shamte Ally, Geoffrey Bonny, Athman Iddi Chugi (Vincent
Barnabas), Kigi Makasi (Abdi Kassim), Boniface Ambani (Gaudence Mwaikimba),
Mrisho Ngassa.
Tusker nayo,
chini ya kocha Jacob ‘Ghost’ Mulee, iliwakilishwa na Boniface Otieno, Ibrahim
Shikanda, John Njoroge, Joseph Shikokoti, Humphrey Okoti, Japhery Oyando
(Crispin Odula), Edward Kauka, Osborne Monday, Simon Mburu, John Kio (Robson
Ndondo), Justus Anene (Hassan Aden).
Sasa kulikuwa
hakuna ujanja, kwani mahasimu hao walikuwa lazima wakutane kwenye mchezo wa
mshindi wa tatu Julai 27. Yanga ikasema isingepeleka timu kwa vile kulikuwa na
hujuma za wazi. Cecafa na wapenzi wengi wa soka wakasema hiyo ilikuwa ‘danganya
toto’ kwa sababu ni kawaida kwa timu hizo kutishia hasa zinapokutana ili
kuichanganya kisaikolojia timu nyingine.
Hatimaye Julai 27
ikafika, mashabiki wakajaa uwanjani wakijua lazima Yanga ingekwenda tu.
Mwamuzi Caleb
Amwayi kutoka Kenya, aliyesaidiwa na Mkenya mwenzake Hesborn Mbogo na Berhe
Tesfagiorgis wa Eritrea, wakasubiri hadi dakika 15 baada ya muda wa mchezo kufika,
zilipopita wakapuliza kipyenga cha kumaliza mchezo na kuipa ushindi Simba.
Siku hiyo kikosi
cha Simba, ambayo kwenye benchi la ufundi ilikuwa na Krasimir Bezinski wa
Bulgaria, na ambacho kilipangwa kucheza na Yanga kilikuwa na Amani Simba,
Kelvin Yondan, Henry Joseph, Musa Hassan, Ramadhani Chombo, Juma Jabu, Nico
Nyagawa, Jabir Azizi, Emmanuel Gabriel, Antony Matangalu, na Meshack Abel.
Kutokana na hali
hiyo, siku hiyo hiyo na wakati huo huo, Cecafa wakatangaza kuifungia Yanga
kushiriki mashindano hayo kwa miaka mitatu na wakataka ilipe faini ya Dola
50,000!
Kwenye mchezo wa
fainali, Tusker iliifunga URA mabao 2-1. Mabao ya washindi yalifungwa na ‘Ngongoti’
Joseph Shikokoti dakika ya 71 na Oscar Kadenge dakika ya 88, wakati URA ndiyo
iliyokuwa imeanza kufunga katika dakika ya 23 kupitia kwa Martin Muwanga.
URA iliwakilishwa
na Abbey Dhaira, Tony Mawejje, Manco Kaweesa, Joseph Owino, David Kyobe, Ismail
Kogozi (Robert Okello), Dan Wagaluka, Mussa Docca (John Karangwa), Johnson
Bagoole, Martin Muwanga, Samuel Mubiru.
Tusker
iliwakilishwa na Boniface Otieno, Ibrahim Shikanda, John Njoroge, Joseph Shikokoti,
Humphrey Okoti, Edward Kauka, Osborne Monday, Simon Mburu (Oscar Kadenge), Hassan
Aden (John Kio), Crispin Odula (Kelvin Omondi), na Justus Anene.
Matokeo kamili ya
mashindano hayo ni kama ifuatavyo:
Kundi A (Dar es Salaam)
12 Jul Simba 2-3
Tusker
Wafungaji: Ulimboka Mwakinwe 21, Adam
Kingwande 30; Simon Mburu 9, Oscar Kadenge 45, John Keo 53.
14 Jul Vital'ô 1-2
Banaadir Telecom
Wafungaji: Kabungulu Nimubona 89; Ivan Edward
59, Nune Abdi 90.
16 Jul Tusker 1-3
Vital'ô
Wafungaji: Kenneth Wendo 70; Eric Gatoto 16,
Kabungulu Nimubona 30, Stanley Minzi 67.
17 Jul Simba 5-0
Banaadir Telecom
Wafungaji: Mussa Hassan 45+, 71, Adam
Kingwande 62, Ulimboka Mwakingwe 68, Emeh Izechukwu 88.
20 Jul Tusker 5-0
Banaadir Telecom
Wafungaji: John Njoroge 14, Joseph Shikokoti
22, Jeff Oyando 74, Kenneth Wendo 76, Osborne Monday 83.
20 Jul Simba 1-0 Vital'ô
Mfungaji: Kelvin Yondan 42.
1.Simba 3 2
0 1 8- 3
6 (Tanzania)
2.Tusker 3 2
0 1 9- 5
6 (Kenya)
3.Vital'ô 3 1
0 2 4- 4
3 (Burundi)
4.Banaadir Telecom 3
1 0 2
2-11 3 (Somalia)
Kudni B (Morogoro)
13 Jul URA 4-1
Rayon Sport
Wafungaji: Johnson Bagole 31, 48, Robert
Okello 69, Eric Obua 84; Jimmy Gatete 90.
16 Jul Awassa
Kenema 1-1 URA
Wafungaji: Ftisum Tsegazab 86; Johnson
Bagoole 26.
19 Jul Rayon Sport 2-0 Awassa Kenema
Wafungaji: Jean Lomani 16, Kalisa Kasse 83.
1.URA 2 1
1 0 5- 2
4 (Uganda)
2.Rayon Sport 2
1 0 1 3-
4 3
(Rwanda)
3.Awassa Kenema 2
0 1 1 1-
3 1
(Ethiopia)
Kundi C (Dar es Salaam)
13 Jul Yanga 2-2
APR
Wafungaji: Mrisho Ngasa 65, Jerry Tegete 68;
Mbuyu Twite 15, 77.
15 Jul APR 1-2
Miembeni
Wafungaji: Baptiste Mugiraneza 86; Amri
Kiemba 42, Maulid Ibrahim 72.
19 Jul Young
Africans 1-0 Miembeni
Mfungaji: Kigi Makasi 22pen.
1.Young Africans 2
1 1 0 3-
2 4
(Tanzania)
2.Miembeni 2
1 0 1 2-
2 3
(Zanzibar)
3.APR 2 0
1 1 3- 4
1 (Rwanda)
Robo Fainali (Shamba la Bibi, Dar es Salaam)
22 Jul Simba 2-0
APR
Wafungaji: Orji Obina 80, Mussa Hassan 87.
22 Jul URA 2-0
Miembeni
Wafungaji: Ismail Kigozi 25, Sam Mubiru 71.
23 Jul Yanga 2-0
Vital'ô
Wafungaji: Shamte Ally 14, Boniface Ambani 20.
23 Jul Tusker 0-0
Rayon Sport [7-6 pen - hakuna muda wa ziada]
Nusu Fainali (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)
24 Jul Simba 0-1
URA [dakika 120]
Mfungaji: Eric Obua 111. Penati ya Emeh
Ezechukwu ilidakwa dakika ya 119.
Simba: Amani
Simba, Nico Nyagawa, Ramadhan Wasoo, Kelvin Yondan, Henry Joseph, Anthony
Matangalu (Emeh Izechukwu), Mohamed Banka (Ulimboka Mwakingwe), Ramadhan
Chombo, Obinwa Orji (Adam Kingwande), Meshack Abel, Mussa Hassan
"Mgosi"; Kocha: Kiwelu
Jamhuri.
URA: Abbey
Dhaira, Johnson Bagoole, Manco Kaweesa, Joseph Owino, David Kyobe (Martin
Muwanga), Ismael Kigozi, Mussa Docca, Robert Okello (Jackson Ssenabulya), Dan
Wagaluka, Henry Kiseka (Eric Obua), Samuel Mubiru; Kocha: Moses Basena.
Mwamuzi: Thomas
Onyango (Kenya); Mussie Kinde (Ethiopia), Hesborne Mbogo (Kenya).
25 Jul Yanga 0-1
Tusker
Mfungaji: Simon
Mburu 53.
Yanga: Ivo
Mapunda, Shadrack Msajigwa, Wisdom Ndhlovu, George Owino, Nurdin Bakari, Shamte
Ally, Geoffrey Bonny, Athman Iddi Chugi (Vincent Barnabas), Kigi Makasi (Abdi
Kassim), Boniface Ambani (Gaudence Mwaikimba), Mrisho Ngassa; Kocha: Dusan Kondic (Serbia).
Tusker: Boniface
Otieno, Ibrahim Shikanda, John Njoroge, Joseph Shikokoti, Humphrey Okoti,
Japhery Oyando (Crispin Odula), Edward Kauka, Osborne Monday, Simon Mburu, John
Kio (Robson Ndondo), Justus Anene (Hassan Aden); coach: Jacob Mulee.
Mwamuzi: Hudu
Munyemana (Rwanda); Ally Kombo (Zanzibar), Berhe Tesfagiorgis (Ethiopia).
Mshindi wa Tatu (Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam)
27 Jul Simba w/o
Yanga [Yanga iligoma kupeleka timu uwanjani]
Simba: Amani
Simba, Kelvin Yondan, Henry Joseph, Musa Hassan, Ramadhani Chombo, Juma Jabu,
Nico Nyagawa, Jabir Azizi, Emmanuel Gabriel, Antony Matangalu, Meshack Abel; Kocha: Krasimir Bezinski (Bulgaria).
Mwamuzi: Caleb
Amwayi (Kenya); Hesborn Mbogo (Kenya), Berhe Tesfagiorgis (Eritrea).
Fainali (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)
27 Jul URA 1-2
Tusker
Wafungaji: Martin Muwanga 23; Joseph
Shikokoti 71, Oscar Kadenge 88.
URA: Abbey
Dhaira, Tony Mawejje, Manco Kaweesa, Joseph Owino, David Kyobe, Ismail Kogozi (Robert
Okello), Dan Wagaluka, Mussa Docca (John Karangwa), Johnson Bagoole, Martin
Muwanga, Samuel Mubiru.
Tusker: Boniface
Otieno, Ibrahim Shikanda, John Njoroge, Joseph Shikokoti, Humphrey Okoti, Edward
Kauka, Osborne Monday, Simon Mburu (Oscar Kadenge), Hassan Aden (John Kio), Crispin
Odula (Kelvin Omondi), na Justus Anene.
Mwamuzi: Hudu
Munyemana (Rwanda); Ally Juma Kombo (Zanzibar), Hamisi Changwalu (Tanzania).
KUMBUKUMBU
HIZI ZIMEANDALIWA NA MTANDAO WA www.brotherdanny.com. Tafadhali ukirejea weka chanzo cha habari.
No comments:
Post a Comment