APR walipotwaa Kombe la Kagame mwaka 2010.
Na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com
ARMÉE Patriotique Rwandaise F.C. ndiyo timu
pekee ya Rwanda yenye mafanikio makubwa zaidi ndani na nje ya mipaka.
Mtandao wa www.brotherdanny.com unaendelea kuwaletea uchambuzi wa kihistoria katika mashindano
haya ambayo yanafanyika jijini Dar es Salaam.
APR inashiriki mara ya 16 michuano ya Kombe
la Kagame, lakini pamoja na kuanza kushiriki mwaka 1996, timu hiyo imefanya
vizuri kuliko timu nyingi kongwe, ambapo imefika fainali mara 8 na kutwaa
ubingwa huo mara tatu kama ilivyo kwa Gor Mahia ya Kenya,
El-Merreikh ya Sudan na SC Villa ya Uganda.
Timu hiyo ilitwaa ubingwa katika miaka ya 2004,
2007 na 2010 na imecheza fainali katika miaka ya 1996, 2000, 2005, 2013 na
2014. Imeishia nusu fainali mwaka 2006 na 2012, na robo fainali mwaka 1997 na
2008 na katika miaka 2001 na 2011 iliishia kwenye makundi.
Ukiangalia takwimu za mafanikio ya miaka
yote kwenye mashindano hayo, APR ndiyo ya tatu kwa kucheza mechi 75, kushinda
40, sare 12 na kufungwa mechi 18 huku ikipachika mabao 133 na kufungwa 69.
Timu hiyo imepata kuwa na wachezaji mahiri
kama Hamisi Bagumaha, Lulenti Kyeyune, Nino Kalisa, Eric Nshimiyimana, Millie
Hassan, Olivier Karekezi, Muhaimana Theonest, Jimmy Gatete, Ndizeye Aimé,
Bizimana Didier, James Kayimba, Titus Mulama, Loman Ahore, Ssozi Philip, Hamis
Yusuf, Yusuf Kayifura, Elius Ntaganda, Bobo Bola, George Waweru, Manfred Kizito,
Kadogo Alimas, Abdu Sibomana, Claude Ndoli, Tabula Aboubakar, Alwa Gaseruka, Sadou
Boubaker, Kizito Manfred, Vincent Kayizi, Andre Lomani, Rafiki Bob, Abbas Rasoo,
Joseph Bwalya, Laurent Kabanda, Almasi Kadogo, Sibomanda Abdul, Elias Ntaganda,
na wengineo.
Kwa sasa kikosi hicho kinachonolewa na
Mserbia Ljupko Petrovic anayesaidiwa na Eric Niyonshima, kinaundwa na wachezaji
kama Kwizera Olivier, Michel Rusheshangoga, Albert Ngabo, Migi Mugiraneza, Emery
Bayisenge, Ismael Nshutinamagara, Yannick, Hegman Ngomirakiza, Jean-Claude
Iranzi na Jean-Claude Ndoli.
Historia yake
APR ni timu ya Jeshi la Rwanda ambayo
ilianzishwa rasmi Juni 1993 ikiwa inaundwa na wanajeshi wa Rwandese Patriotic
Front (RPF) kabla hata ya kuinyakua Rwanda.
Uongozi wa klabu hiyo ni wa kijeshi ambapo
Rais wa klabu ni Meja Jenerali Alex Kagame, Makamu Mwenyekiti ni Meja Jenerali HadjMubaraka
Muganga, Katibu Mkuu ni Alain Gakuba, Meneja Uhusiano na IT ni Siboman Abdou,
Ofisa Uhusiano ni Stephen Mupenzi, Meneja wa timu ni mshambuliaji wa zamani wa
klabu hiyo Kapteni Eric Nshimiyimana na daktari ni Luteni Venusté Muratwa,
Kama nilivyosema, pamoja na historia yao
fupi, lakini ndiyo klabu inayoongoza kwa mafanikio kuliko zote nchini Rwanda
ambapo imetwaa ubingwa wa ligi mara 13, Kombe la Rwanda mara saba na Kombe la
Kagame mara tatu.
Mafanikio:
Ubingwa wa Ligi Kuu Rwanda: 14
1995, 1996, 1999, 2000, 2001, 2003, 2005,
2006, 2007, 2009, 2010, 2011, 2012, 2014, 2015
Kombe la Rwanda: 8
2002, 2006, 2007, 2008, 2010, 2011, 2012,
2014
Ubingwa wa Kagame: 3
2004, 2007, 2010
Ligi ya Mabingwa Afrika: Imeshiriki
mara 10
1997 – Raundi ya Kwanza
2000 – Ilijitoa Raundi ya Kwanza
2002 - Raundi ya Kwanza
2004 - Raundi ya Tatu
2006 - Raundi ya Kwanza
2007 - Raundi ya Kwanza
2008 - Raundi ya Awali
2010 - Raundi ya Kwanza
2011 - Raundi ya Awali
2012 - Raundi ya Kwanza
2013 -
Klabu Bingwa Afrika: Mara 1
1996 - Raundi ya Pili
Kombe la Shirikisho: Mara 3
2004 - Raundi ya Kati
2005 - Raundi ya Pili
2009 - Raundi ya Kwanza
Kombe la Washindi: Mara 1
2003 – Nusu Fainali
Kombe la CAF: Mara 2
1998 - Raundi ya Kwanza
1999 - Raundi ya Kwanza
KUMBUKUMBU HIZI ZIMEANDALIWA
NA MTANDAO WA www.brotherdanny.com. Tafadhali ukirejea weka chanzo cha habari.
No comments:
Post a Comment