
Na Hastin Liumba, TaboraZoezi la Uandikishaji wapiga kura linaloanza katika Manispaa ya Tabora hivi karibuni linaweza likaingia dosari kutokana na upungufu wa kadi za kupigia kura na uchache wa vituo vya kuandikishia wapiga kura.
Akizungumza na waandishi wa habari Msimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa Frank Mkoga alisema kuwa manispaa hiyo ina jumla ya wananchi wanaostahili kupiga kura 130,686.
Mkoga alisema hadi sasa kadi ambazo zimeletwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni 50,000 wakati zoezi la uandikishaji linaanza Mei 21, 2015 katika kata nane za nje za manispaa hiyo.
Afisa Uchaguzi huyo alisema kuwa lengo lilitakuwa kuwa vituo 295 vyakujiandikisha, lakini cha kushangaza Tume imepitisha vituo 221.
Mbali ya kasoro hizo pia mashine za kielekroniki za kuandiklishiawapiga kura (BVR) zilizopo ni 54 kwa ajili ya kazi ya zoezo hilo,hali inayoonyesha wazi kwamba zoezi hilo litakwama ukizingatia uzoefu wa waandikishajiwamepewa mafunzo ya siku mbili tu.
Hata hivyo afisa uchaguzi wa Manispaa ya Tabora alisema wananchiwahamasishwe kujitokeza kujiandikisha katika muda uliopangwa, kwa sababu hawatarajii kuongeza muda tofauti na huo uliopangwa.
Wananchi wote katika mkoa huu wametakiwa kujitokeza katika zoezi hilo la kujiandikisha kwani wasipojiandikisha hawatapata muda mwingine na kadi hizo zitakuwa vitambulisho vyao vinavyowatambulisha kuwa ni raia wa Tanzania.
Kutokana na dosari hiyo baadhi ya vyama vya siasa vimelalamika na kuomba muda uliowekwa wa siku saba kwa kila kituo cha uandikishaji katika kila kata kuongezwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Cristopha msuka alisema kuna changamoto nyingi kwanza kwa uhaba wa matangazo kwa wananchi ni hafifu sana na hata wengi wa wananchi hawajajua siku ya kujiandikisha.
Msuka vituo vya kujiandikishi ni vichache kiasi kwamba wananchi wa vijijini watatembea umbali mrefu sana kutafuta vituo vya kujiandikishia na wakikuta watu ni wengi wakiondoka hawatorudi tena kujiandkisha kwa muonekano huo watu watakosa fursa za kujiandikisha kutokana na umbali.
Alisema kuwa zoezi hilo limegubikwa na usiri mkubwa na ubabaishi mwingi nakusababisha kukosa imani kwa tume na kufanya uchaguzi mkuu uwe na mashaka.
Mwenyekiti huyo alisema Kama kuna uwezekano tume itumie busara kuhakikisha watu wote wanapata haki ya kujiandikisha kwe daftari la wapiga kura.
No comments:
Post a Comment