
Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Venance Mwamoto
Na Hastin Liumba, KaliuaSERIKALI Wilaya ya Kaliua imesema Mfuko wa afya ya jamii (CHF) siyo jambo la kisiasa bali hilo ni swala linalogusa maisha ya wananchi na si kundi la watu fulani.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Venance Mwamoto wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa afya ya Jamii (CHF) na siku ya wadau ya mfuko huo iliyofanyika wilayani humo.
Alisema kwamba maisha ya wananchi ndio yayotakiwa kukombolewa na sio kuweka mambo ya kisiasa katika uhai wa binadamu na kufanya hivyo kutasababisha kundi kubwa la watu wagonjwa katika wilayani humo .
Alisema kwamba taifa linajali maisha ya wananchi wake na kuweka utaratibu wakuweza kutibiwa kwa kadi na sio kulipa kila unapoumwa kwani kufanya hivyo kutasababisha jamii kuendelea kuwa na maradhi .
Mkuu huyo wa wilaya aliendelea kusema kwamba mfuko wa afya ya jamii ni kinga kubwa ambayo inapunguza vifo vya wananchi wake na mwisho wa siku taifa bila maradhi litawezekana .
Mwamoto alisema kwamba zoezi la uchangiaji matibabu likifanyika vizuri na dawa zikipatikana za kutosha katika zahanati, vituo vya afya na hospitali kutakuwa na ugumu wa wananchi kuchangia huduma zao za tele kwa tele.
Awali mganga mkuu mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt Gunii Kamba alisema kwamba mfuko wa afya ya jamii ni mkombozi wa wananchi wote katika kupata tiba kila siku kwa kutoa kiasi cha shilingi 5000 na serikali kuongeza kiasi kama hicho.
Alisema kwamba jamii ikielimishwa vizuri katika jambo hilo basi wilaya nzima ya Kaliua hadi kufikia mwisho mwa mwaka huu kila kaya itakuwa na kadi ya CHF kwa ajili ya Tiba katika zahanati,viyuo vya afya na Hospitali ya Wilaya ya Kaliua .
Alisema kwamba inawezakana kufanyika hata kwa Mkoa wa Tabora kuweza kutumia kadi hizo katika hospitali za Rufaa na wilaya kwa wilaya za mkoa huo kwa lengo la kupunguza vifo visivyotarajiwa .
“Jambo hilo linawezaka iwapo tutaweka mikakati ya pamoja kwa ajili ya kuhoko maisha ya wananchi wa mkoa wa Tabora hasa wale waliopo vijijini kwani kila siku gharama za maisha zinapanda kwa kufanya hivyo tutaokoa misha ya watu wengi hasa mama wajazito”alisema Dkt Kamba.
No comments:
Post a Comment