Fikiria anakwenda mjini akiwa na mfuko wa Rambo, ndani ameiviringisha bunduki ya kivita na rambo nyeusi kiasi kwamba ni vigumu kubaini amebeba nini.
Anapofika kwenye 'uwanja wa mapambano' anaichomoa vivyo hivyo na kuikumbatia barabara.
Hakika huwezi kukatiza mbele yake, maana yaonekana kabisa anajua namna ya kuitumia.
Haya ni mambo ya Burundi siku ya jaribio la mapinduzi, kila mmoja yuko tayari kwa lolote.
Vita tuvisikie tu kwa wenzetu, hakuna sister duu atakayebaki salon akijipodoa, wala brother men watakaovaa suruali kwenye 'gear box'. Inatisha jamani, tuwaombee wenzetu amani.
No comments:
Post a Comment