Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 18 May 2015

KAMATI YA SIASA CCM TABORA YAMTOSA KATIBU


Na Mwandishi Wetu, Tabora
WAJUMBE wa kamati ya siasa na wajumbe halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini kwa kauli moja imeomba kamati ya maadili ya chama hicho toka makao makuu Dodoma kuwa katibu  CCM wilayani hapo Bakar Lwasa akabidhi ofisi hawamtaki kutokana na tuhuma mabalimbali zinazomkabili, imefahamika.


Habari toka ndani ya kikao cha kamati ya maadili ya chama hicho toka makao makuu zinasema nayo kamati ya siasa wilaya kwa kauli moja imemkataa Lwasa kwa tuhuma mbalimbali za kukigawa chama na upotevu wa fedha.
Wajumbe wa kamati hiyo ndogo iliwasili siku ya Alhamis ya mwezi Mei 14,2015 kwa ajili kusikiliza mgogoro huo baada wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini kuandamana hadi ofisi ya katibu wa CCM mkoa Janeth Kayanda wakitaka aondoke.
Hata hivyo mwezi Mei 16 mwaka huu kamati hiyo ilikutana na kamati ya siasa na kuongelea mgogoro huo bila mafanikio na kulikuwepo na ushawishi wa kamati hiyo wajumbe wa kamati ya siasa wasameheane lakini ilishindikana.
Aidha chanzo kinasema kikao kilimalizika kwa kutopata muafaka hali ambayo inaonyesha katibu wa chama hicho Bakar Lwasa safari imeiva.
Mapema majira ya saa tatu asubuhi kundi linalomuunga mkono Bakar Lwasa lilifika ofisi za CCM wilaya Tabora mjini likitaka kuweka ushahidi kwa kamati hiyo juu ya kusulubiwa katibu huyo lakini almanusura zipigwe ngumi kavukavu.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa walisema tuhuma za katibu huyo zinatosha yeye kuondoka kwani kama kuna mtu anambeba basi na yeye asubiri wakati wake aondoke kwani CCM kila kukicha inadhofu.
Gazeti hili lilifika eneo la mkutano na kukuta baadhi ya wajumbe wakiwa nje na wengine wakiwa ndani ya ukumbi na baada ya majira ya saa nane alasili kikao hicho kilimalizika.
Aidha wajumbe kadhaa walisema tumeamua katibu aondoke lakini sisi siyo wasemaji na kukueleza kamati hiyo iliongozwa na nani ikiwa na watu wangapi hatuwezi kukukwambia tunasubiri majibu ya CCM taifa.
Madai ya katibu kuhusu tuhuma zake ni baadhi ya wajumbe na risala ya wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya Tabora mjini ni upotevu wa Shs. 8 milioni na kukigawa chama.
Tuhuma zingine ni kusababisha makundi yanasigana hadi sasa na kusababisha chama kuyumba kutokana na makundi hayo.
Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Janeth Kayanda alisema hawezi sema chochote,huku mwenyekiti wa CCM mkoa Hassan Wakasuvi akisema hana chochote kile aulizwe siku ya jumatatu hana majibu kwa muda huo.
 Kwa upande wake katibu aliyekataliwa Bakar Lwasa majibu yake yakiwa hana cha kusema yeye ni msimamizi wa kanuni  za Chama.
mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini Abdulrahaman Nkonkota alijibu hawezi kuzungumzia kikao hicho tuwe na subira kwanza hadi hapo baadaye kwani ni siri za kikao.
Hadi tunakwenda mitamboni kamati hiyo haikufahamika ni nani walikuja kusikiliza mgogoro huo.

No comments:

Post a Comment