Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 21 May 2015

CHADEMA WAIJIA JUU SERIKALI KUHUSU RIPOTI YA CAG


NA ISAYA KISIMBILU
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimedai kupokea kwa masikitiko taarifa za ufisadi wa kutisha uliofanyika kwenye matumizi ya fedha za umma kama ilivyobainishwa kwenye ripoti za ukaguzi wa fedha kwa mwaka 2013/2014 kupitia Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

 
Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho, Sh. trilioni 1.151 sawa na asilimia 5.231 ya bajeti yote ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha 2015/16 inayoendelea kujadiliwa, zimepotea au kuliwa na watendaji wasiowaaminifu serikalini. “Ripoti ya CAG iliyotolewa inaonyesha kuwa katika serikali kuu, wizara tatu tu ambazo tumezifanyia uchambuzi mpaka sasa ambazo zimepoteza kiasi cha Shilingi 1.151 trilioni,” ilisema.
 
Taarifa hiyo ilizitaja baadhi ya wizara hizo kuwa ni Wizara ya Fedha kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa madai ya kwamba  fedha zilizopotea kutokana na bidhaa ambazo zilipaswa kuuzwa nje ni kutokana na uzembe hivyo kuuzwa ndani ya nchi bila kulipiwa kodi ambazo ni Sh. bilioni 836. 
 
Pia Ofisi ya Waziri Mkuu , kitengo cha maafa ambako zilidaiwa kupotea jumla ya Sh. bilioni 163 huku  Wizara ya Ujenzi  zikidaiwa kupotea Sh. bilioni 252.
 
 “Mwaka 2013/14 yalifanyika  maboresho ya sheria mbalimbali za kodi wakati wa bunge la bajeti, kodi ambazo kimsingi zilimwongezea mwananchi mzigo mzito wa kulipia kwa ajili ya kuongeza mapato ya serikali ili kuiwezesha kuwahudumia wananchi wake. Pamoja na ongezeko hilo la kodi, fedha yote iliyokusanywa katika mwaka wa fedha 2013/14  imepotea yote katika wizara tatu tu za serikali kutokana na vitendo vya kifisadi,” ilifafanua.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment