Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 4 May 2015

SKIKA PROGRAMME TANZANIA KUSAMBAZA SOLAR

Na Hastin Liumba, Tabora
SHIRIKA lisilo la kiserikali la SKIKA Programme Tanzania limelenga kusambaza umeme wa jua (Solar) kwa kaya zipataza 3,000 mkoani Tabora.


Mkurugenzi wa shirika hilo Peter Mkufya alisema hayo kwenye uzinduzi wake mkoani Tabora na kushirikisha makundi mbalimbali ya kijamii.


Mkufya alisema hatua ya shirika hilo itasaidia zaidi katika kupunguza matumizi ya umeme,mafuta ya taa na kupunguza zaidi nishati ya kuni ambayo imekuwa ikisababisha uharibifu wa mazingira.


Alisema mazingira kila kukicha yanaharibiwa kwa matumizi ya kuchoma mkaa,kuni na matumizi mengine ambayo kwa kiasi kikubwa yanahatarisha uhai wa mazingira na taifa kugeuka jangwa.


Mkufya alisema kutakuwa na aina mbalimbali za vifaa vya umeme huo na kwamba mradi umelenga sekta za Elimu,Afya na Kilimo.


Alisema ana imani zaidi kuwa maendeleo yoyote yanategemea nishati ya umeme hivyo jibu sahihi la mbadala wa matumizi ya nishati ya umeme ni umeme huo.


Aidha licha ya hivyo pia alibainisha matumizi ya umeme watakaosambaza pia utapunguza zaidi ajali zitokanazo na ajali za moto hasa kwa matumuzi ya Mishumaa na Koroboi (Vibatari).


Alisema utafiti unaonyesha kuwa matumizi ya Mafuta ya Taa lita moja ya matumizi yanasababisha uwepo wa kilo mbili za hewa ya Carbon Dioxide.


Aidha alibainisha vifaa vitakavyouzwa na shirika hilo vitakuwa chini ya uangalizi wa muda wa miaka miwili.


Alisema mradi huo umelenga kusambaza umeme wa juma (Solar) kwa mikoa ya Dar-es-Salaam,Pwani na Tabora.

No comments:

Post a Comment