Mkuu
wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester
Riwa akiongea na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Bw. Martin
Mtani wakati wa ziara ya mafunzo ya ujasiriamali na jinsi ya kujikomboa
kiuchumi kwa Vijana wa Halmashauri hiyo mkoani Ruvuma.wa kwanza kushoto ni
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina
Sanga.(Picha na Benjamin Sawe-WHVUM).
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Bw. Martin Mtani akisisitiza
jambo kwa timu ya wataalam kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo wakati wa ziara ya mafunzo kwa vijana wa Wilaya hiyo yenye lengo la
kuwakwamua kiuchumi.(Picha na Benjamin
Sawe-WVUM)
Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa akiongea na Vijana wa Halmashauri
ya Wilaya ya Namtumbo juu ya umuhimu wao wa kujishughulisha na ujasiriamali ili
kukuza uchumi wa taifa na kujikomboa kiuchumi.(Picha na Benjamin Sawe-
WHVUM)
Afisa
Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga
akitoa mada ya jinsi ya mfuko wa Vijana unavyoweza kuwasaidia vijana wa
Halmashauri ya Namtumbo Mkoani Ruvuma wanaokidhi vigezo vya ujasiliamali ili
kujiinua Kiuchumi.
Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Namtumbo akitoa
mada kwavijana wa Halmashauri hiyo juu ya uanzishwaji wa Saccos ikiwa ni juhudi
za Serikali kuwainua vijana kiuchumi.(Picha
na Benjamin Sawe- WHVUM).
Na Benjamin Sawe, Namtumbo-WHVUM
Serikali
imewaasa vijana kujiepusha na ngono zembe ikiwa ni pamoja nakujiepusha na matumizi
ya dawaza kulevya ili waweze kujiletea maendeleo yao na kujiinua kiuchumi.
Rai hiyo
imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
wakati wa mafunzo elekezi ya jinsi ya kujikwamua kiuchumi kwa vijana wa halmashauri
ya Wilaya ya Namtumbo.
Alisema vijana kujihusisha na ngono zembe na matumizi
ya dawa za kulevya kutawafanya kuwa dhaifu na kushindwa kuchangia katika ujenzi
wa taifa na kujiinua kiuchumi.
“Nawashauri
msijihusishe na ngono zembe na matumizi ya dawa za kulevya kwani mikopo mtakayoipata
mtashindwa kuirejesha kwa wakati hivyo mtaisababishia serikali hasara kubwa”.Alisema.
Bibi.Riwa
amesema kuwa jitihada za awali zifanywe na vijana wenyewe kwakuwa na mwamko wakuleta maendeleo yatakayotokana na
miradi endelevu na yenye malengo kwani kwakufanya hivyo wataweza kukabiliana na
hali ya maisha ya duni na kuwa mfano katika jamii na taifa kwa ujumla.
Aidha
Afisa Maendeleo ya Vijana Wilaya ya Namtumbo Bi.Rahiya Nasser.amewataka vijana wa
Namtumbo kutokupenda kubebwa kwakupewa fedha
za bure kwakununuliwa na wanasiasa bali wazidi kujijengea mazoea ya kuwekeza na
kuchukua mikopo inayotolewa na Serikali kwa vijana yenyeribana fuu na kurejesha
fedha hizo kwa wakati ili vijana wengine waweze kufikiwa na fursa hiyo.
Akizungumza
na vijana wakati wa semina hiyoAfisaUshirika Halmashauri yaWilaya ya hiyo Bw.
Theophily Ngonyani amewataka vijana kutokuwa watu wakusukumwa kutafuta maendeleo
yao bali wawajibike nakutafuta fursa zilizopo ili kuweza kuondokana na hali
duni ya maisha.
“Vijana
wenzangu hamjazaliwa kuishia hapo mlipo, msipende kusukumwa nawatu kutafuta maendeleo
yenu ,changamkieni fursa zilizopo nakuwajibika katika jamii
zenu bila ya kuwa na ubaguzi wakijinsia kwaniNamtumbohaitakiwi kuwa kama ilivyo
sasa” alisemaBw. Ngonyani.
No comments:
Post a Comment