IGP Ernest Mangu
Na Mwandishi Wetu, Tabora
JESHI
la polisi mkoani Tabora limelalamikiwa na kutuhumiwa kwa kumbambika
kesi Bilali Saidi Masangura ya wizi wa TV na sh milioni 200.
Akiongea
muda mfupi kituo kikuu cha polisi mkoani Tabora kabla ya kupelekwa
wilayani Urambo anakotuhumiwa wizi wa TV alisema hana hatia juu ya kesi
hizo mbili.
Bilali Masangula alisema alikamatwa mkoani Morogoro akiwa njiani kuelekea Dar-es-Salaam katika biashara zake za mahindi.
‘Nilikuwa
safarini toka Mwanza kuelekea jijini Dar-es-Salaam katika biashara
zangu nilikamtwa nikaletwa mkoani Tabora na kufunguliwa kesi hizo,"
alisema.
Alisema
baada ya kukamatwa alirejeshwa mkoani Tabora na kufunguliwa mashitaka
ya wizi wa sh milioni 200 za kampuni moja (jina linahifadhiwa).
Aidha alibainisha kuwa kesi hiyo ilifanyiwa uchunguzi wa kina na mwisho wa siku ilionekana sina hatia na kesi kufutwa.
Alisema baada ya kufutwa kwa kesi hiyo ghafla tena alikamatwa na kufunguliwa kesi nyingine ya wizi wa TV wilayani Urambo.
Aidha
alisema kesi hiyo amefunguliwa baada ya kusota rumande kwa siku 23 bila
ya kupelekwa mahakani huku akinyimwa dhamana na kupewa vitisho.
Alisema
yeye biashara zake ni Mahindi na ana duka la simu za kiganjani anauza
"sasa huo wizi ninaotuhumiwa ni njama za baadhi ya polisi kunibambika
kesi."
Alisema
anasikitishwa na polisi hao kwani dhamana alinyimwa huku akisota
rumande siku 23 bila kupelekwa mahakamani kama sheria zinavyosema.
Alisema ameamua kuongea na waaandishi wa habari ili umma ujue uonevu anaotendewa na polisi akiwa hana kosa lolote.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi (ACP) Suzan Kaganda
alipoulizwa malalamiko hayo alisema hana taarifa za Bilali Masangura
kubambikwa kesi.
Kamanda
Kaganda alisema licha ya kutokuwa na taarifa hizo atafuatilia lakini
akasema hakuna ndugu wala huyo Bilali aliyewasilisha malalamiko kwake.
‘Sijaona
mtu yoyote wala hao wanaolalamika kubambikwa kesi ili niweze kuchukua
hatua zaidi……waje tu kuniona niweze kujua nini kinaendelea,” aliongeza.
No comments:
Post a Comment