Manny Pacquiao (kulia) na Floyd Mayweather (kushoto) kabla ya pambano
Manny Pacquiao ameshutumiwa kwa kudanganya kuwa alikuwa akiumwa bega kabla ya pambano dhidi ya Floyd Mayweather. Pambano hilo lilipigwa Las Vegas, Marekani.
Iwapo Mfilipino huyo atakutwa na hatia, adhabu atakayopata kwa mujibu wa sheria itakuwa kifungo jela cha kati ya mwaka mmoja na miaka minne, na faini ya kufikia dola za Kimarekani $5,000 (£3,305).
Tume ya Michezo ya Nevada, NAC, imesema Pacquiao, mwenye umri wa miaka 36, hakutangaza kuwa majeruhi katika fomu ya maelezo kabla ya pambano.
Lakini Pacquiao anasema alikuwa muwazi na mpango wa matibabu ulikuwa umekubaliwa.
Pacquiao alisema kupigwa kwake kumetokana na maumivu - akidai kuwa alishindwa kutumia mkono wake wa kulia katika pambano hilo- lakini taarifa ya pamoja iliyotolewa na Team Pacquiao na mapromota wake Top Rank imesema Shirika la Marekani la Kuzuia Matumizi ya Dawa za Kuongeza Nguvu Michezoni, Usada, lilijulishwa juu ya sula hilo wakati wa kambi ya mazoezi ya mwanamasumbwi huyo na pia katika usiku wa pambano.
Wamesema daktari mmoja wa Usada alizuia matumizi ya dawa moja ya kuzuia maumivu usiku wa pambano, lakini NAC haikuruhusu kutolewa kwa sababu hawakujua kuhusu kuumia bega.
Taarifa hiyo imesema: "Hii inakatisha tamaa kutokana na ukweli kwamba Team Pacquiao ilieleza kuhusu Pacquia kuumia bega na matibabu kwa Usada, ambao waliidhinisha matibabu na Manny aliorodhesha dawa katika fomu yake ya kabla ya pambano."
NAC imesema kambi ya Pacquiao haikulazimika kueleza kuhusu kuumia kwa bondia wake, lakini mkurugenzi mtendaji wao Bob Bennett amesema: "si tu kwamba hakujaza fomu kikamilifu,ni kwamba hakuwa mwaminifu. "Saa mbili kabla ya pambano walitaka dawa ya kutuliza maumivu. Suala hilo lilituweka katika mazingira magumu sana."
CREDIT: BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment