Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Ester Riwa mbele akionyesha Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka
2007 wakati wa mafunzo ya elimu ya Ujasiriamali, Mfuko wa Vijana, Stadi za
Maisha na Uongozi bora kwa Vijana wa Halmashauri ya Tunduru.
Afisa
Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga
aliyeshoosha mkono akiwa katika ukaguzi wa mradi wa kikundi cha Hatubanani
kilichopo Halmashauri ya mji wa Tunduru kinachojishughulisha na duka la uuzaji
wa vinywaji baridi, mradi wa kikundi hicho umepata mkopo wa shilingi milioni
nne kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana.wa kwanza kushoto ni katibu wa kikundi
hichi Bi Hawa Mayanga na kulia ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Vijana Sasanda
kilichopo Mkoani Mbeya Bw. Laurian Masele.
Maafisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa
katika ukaguzi wa mradi wa ufugaji samaki kilichopo Halmashauri ya mji wa
Tunduru wakati wa mafunzo kwa vijana ya kuwakwamua kiuchumi.Katikati ni Afisa
Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga
kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Vijana Sasanda kilichopo Mkoani Mbeya
Bw. Laurian Masele.
Vijana
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga
aliyeshoosha mkono akitoa mada ya jinsi ya utendaji kazi wa Mfuko wa Maendeleo
ya Vijana wakati wa mafunzo ya kuwakwamua vijana wa Halmashauri ya Tunduru kiuchumi.
Na Benjamin
Sawe, Tunduru
Jamii imetakiwa kuwa na nidhamu ikiwa ni pamoja na kuwa na usimamizi
mzuri katika shughuli za kujiletea maendeleo.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kwa wajasiriamali vijana
wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Manfred
Hyera amesema chanzo cha mafanikio katika ujasiriamali nikuwa na nidhamu kwa jamii
inayowazunguka kwani kwa kufanya hivyo kutawawezesha kuwaongezea kipato.
Bw.Hyera amesema kitendo cha baadhi ya wajasiriamali kutumia lugha chafu kwa wateja ndio chanzo kinachowarudisha
nyuma na kufilisika kibiashara.
“Baadhi ya wajasirimali mnatumia lugha chafu kwa wateja wenu
hiki ni chanzo kikubwa cha kufilisika kibiashara na kubaki kuilalamikia serikali”.Alisema.
Alisema serikali kupitia WizarayaHabari, Vijana, Utamaduni na
Michezo inaniayadhati yakushirikiana na wanachi wote hususani Vijana ilikukabiliana
na tatizo la ajira nchini.
Katika hatua nyingine AfisaVijana Bi. Amina Sanga amewashauri
vijana kuwa wabunifu ili kuendana naushindani
wa soko la biashara unaoendelea nchini na duniani kwa ujumla.
Akitolea mfano wa ujenzi unaoendelea wa barabara kwa kiwango
cha lami Bi. Sanga alisema ni fursa mojawapo kwa vijana wa Halmashauri hiyo kubuni
biashara ambayo itawaingizia kipato kiurahisi kwani kwa kukamilika
kwabarabara hiyo kutakuza uchumi wa maeneo ya Wilaya ya Tunduru.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa amewashauri vijana hao kuweka
itikadi za siasa pembeni kwani serikali yao hushirikiana vijana wote bila ubaguzi
wa dini au kabila.
No comments:
Post a Comment