Mlinzi wa Jaji Joseph Warioba (kushoto) akimkinga kwa mikono ili asipate madhara baada ya mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa kuvamiwa na kundi la vijana na kusababisha uvunjifu wa amani.
Mtoa mada katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa,
Jaji Joseph Warioba akitoa mada kabla ya mkutano huo kuvunjika katika ukumbi wa
Ubungo Plaza jijini Dar es Saam leo. (Picha zote na Francis Dande)
Baadhi ya vijana walioingia na mabango ndani ya ukumbi wa mkutano
wakiwa na mabango yaliyokuwa yakisomeka ‘Katiba inayopendekezwa tumeipokea
tunaiunga mkono’
Jaji Joseph Warioba akiangalia usalama wake kabla ya kuondolewa mlinzi
wake katika ukumbi wa Ubungo Plaza ambapo mdahalo wa kuijadili Katiba
inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika kabla ya kuvunjika.
Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole akimzuia mmoja wa vijana
aliyekuwa na jazba mara baada ya kutokea kwa vurugu katika mdahalo wa kujadili
Katiba inayopendekeza.
Mkurugenzi wa Taasisi ya
Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku (katikati) akisindikizwa
kuingia katika chumba cha VIP mara baada ya kuvunjika kwa mdahalo wa kujadili
Katiba inayopendekezwa. Mdahalo huo uliandalia na taasisi hiyo.
Jaji Joseph Warioba akitoa mada.
Vijana wakiwa na mabango.
Mabango yakiwa juu.
Fujo zinaanza.
Mmoja wa vijana waliokuwa wakitoa maneno ya kashfa kwa Jaji Warioba akiwanyooshea vidole viongozi wa meza Kuu.
Baadhi ya viti vilivyovujwa.
Jaji Warioba akitoka katika ukumbi huku akisindikizwa na askari kanzu.
Jaji Warioba akisindikizwa na makachero wa Polisi.
Jaji Warioba akiwapungia mkono wananchi waliokuwa wamefurika nje ya jengo la Ubungo Plaza ambako mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika.
Wananchi walikuwa nje ya jengo la Ubungo Plaza wakimshangilia Jaji Warioba wakati akitoka katika ukumbi wa mdahalo huku wakimuita 'Rais Rais'.
Jaji Joseph Warioba akitoa mada.
Vijana wakiwa na mabango.
Mabango yakiwa juu.
Fujo zinaanza.
Mmoja wa vijana waliokuwa wakitoa maneno ya kashfa kwa Jaji Warioba akiwanyooshea vidole viongozi wa meza Kuu.
Baadhi ya viti vilivyovujwa.
Jaji Warioba akisindikizwa na makachero wa Polisi.
Jaji Warioba akiwapungia mkono wananchi waliokuwa wamefurika nje ya jengo la Ubungo Plaza ambako mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika.
Wananchi walikuwa nje ya jengo la Ubungo Plaza wakimshangilia Jaji Warioba wakati akitoka katika ukumbi wa mdahalo huku wakimuita 'Rais Rais'.
Baada ya vurugu hizo, mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kurushwa moja kwa moja na ITV umesimamishwa kwa muda.
No comments:
Post a Comment