Mara Baada ya Ibada katika Kanisa la Azania Front wakati wa kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya amewaomba watanzania kuwa na tabia ya utii wa sheria, uaminifu na uadilifu katika nafasi zao wanazozitumukia katika Taifa la Tanzania.
Msuya aliyasema hayo katika sherehe ye kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya iliyofanyika katika Hotel ya Protea , Court Yard jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu alieleza kuwa tabia aliyoionyesha Mgaya wakati wa utumishi wake serikalini inapaswa kuigwa na watanzania wote.
“Huyu ndiye Mtanzania halisi aliyelelewa vizuri kuitumikia nchi yake. Hana makuu, ni mkweli na mwadilifu. Akiahidi kufanya jambo fulani analitekeleza bila kuchelewa. Tunahitaji uwajibikaji wa namna hii,” Msuya alisisitiza.
Alisema kuwa Mgaya alikuwa kiongozi hodari ambaye alisimamia vyema kiapo na kazi zake na kipindi chake cha uongozi alikuwa akitoa amri zinatekelezwa mara moja.
Naye Mshauri wa kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited James Rugemalira alitoa wito kwa watanzania kuendele kuunga mkono jitihada za kuendeleza maeneo mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo viwanda.
Aliwasihi wadau kutoa ushirikiano kwa kampuni yake inayosambaza bia aina ya Windhoek Larger na Windhoek Draught ambayo inadhamira ya kujenga kiwanda cha kuzalisha bia hizo hapa nchini.
“Tunatafuta maeneo Kilimanjaro, Tanga na Bukoba ili tuweze kujenga kiwanda hapa nchini. Tumedhamilia kufanya hivyo na tutafanya,” Rugemalira alisisitiza.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Benedicta Rugemalira aliwashukuru wananchi kwa kukubali kujumuika pamoja katika hafla hiyo na kumwomba Mzee Mgaya aendelee kuwapa mwongozo wa namna ya kuenenda katika maisha.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Alex Malasusa aliwaomba watanzania kuwa na moyo wa unyenyekevu na kujitolea kulitumikia taifa katika utumishi wao kama ilivyokuwa kwa IGP mstaaafu Mzee Mgaya.
Wageni wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Waziri wa Habari na Utangazaji Fenera Mukangara, Katibu Mkuu Msaaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Bakari Mwapachu, Balozi Antoni Nyaki na wazee wengine maarufu kama Timothy Msangi.
Baadhi ya waumini mbalimbali wakiwa nje baada ya Ibada
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Mstaafu Philemoni Mgaya akiwa katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake
Keki
Waziri Mkuu
Mstaafu Cleopa Msuya akimpongeza aliyekuwa IGP Philemoni Mgaya
Mzee Timothy Msangi akieleza Historia fupi ya IGP Mstaafu Philemoni Msangi
Askofu Mkuu
wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Alex Malasusa akitoa salam za Pongezi kwa IGP mstaafu
Mshauri
wa kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited
James Rugemalira akitoa pongezi zake kwa IGP Mstaafu na kuelezea Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hiyo Benedicta Rugemalira akitoa salamu za Pongezi kwa IGP mstaafu
Waziri wa Habari na Utangazaji Fenera Mukangara akimpa mkono wa Pongezi IGP mstaafu
Wakiwa katika Furaha
Watu mbalimbali wakiwa katika Sherehe hiyo
Burudani ya nguvu
No comments:
Post a Comment