Magare John Shibuda, Mbunge wa Maswa Magharibi (Chadema)
Na Elizabeth Zaya
Mbunge wa Maswa Mashariki Sylivesta Kasulumbai (Chadema), amemshukia Mbunge wa Maswa Magharibi John Shibuda (Chadema) kwamba amewatelekeza wananchi wake kwa kutotekeleza ahadi alizowaahidi.
Kadhalika, amesema Shibuda mbali na usaliti kwa wananchi, lakini pia ni msaliti wa chama chake hususani kwa kusaliti maoni ya wananchi waliyoyatoa kwa iliyokuwa tume ya mabadiliko ya Katiba.
Akihutubia wakazi wa Kata ya Malampaka,katika ziara ya Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Kasulumbai alisema Shibuda amekuwa kama kinyonga ambaye wakati wote huweza kubadilika.
Kasulumbai alisema kwa kitendo ambacho Shibuda amekionyesha kwa wananchi wake na chama chake hawako tayari kumpa nafasi tena.
Kasulumbai ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa Mashariki inayoundwa na mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara, alitumia nafasi hiyo kuwatangazia vijana na mtu yeyote wa Chadema ambaye yuko tayari kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo hilo kujiandaa mara moja kuwania jimbo hilo.
“Shibuda amewasaliti wananchi wake, amesahau wananchi walimwamini wakampa kura akashinda kwa kishindo lakini hajaja hata kuwatembelea, ameshindwa kutekeleza ahadi za wananchi amewaacha kama yatima,” alisema na kuongeza:
“Ni adui namba moja wa maendeleo ya wananchi, anajikomba komba kwa vigogo na kusababisha maendeleo mengi ya wananchi kukwama, nilikuwa mmojawapo wa watetezi wake kipindi chama kilipotaka kumwadhibu kutokana na matendo yake hayo, lakini kwa sasa nimechoka na ninasema bora aadhibiwe na nawatangazia vijana na mtu yeyote wa Chadema anayetaka kugombea jimbo hili ajiandae.”
Mwenyekiti mstaafu wa baraza la vijana la Chadema (Bavicha), John Heche, alisema kwa usaliti ambao Shibuda ameifanya ni halali yake kuadhibiwa na chama.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment