Viongozi wa jeshi nchini Burkina Faso wamemuunga mkono Kanali Issac Zida kama kiongozi wa serikali ya mpito nchini humo.
Taarifa hiyo inaonekana kumaliza tofauti kuhusu ni nani aliyemrithi Rais Blaise Campaore ambaye alijiuzulu kufuatia maandamano ya kumpinga.
Luteni kanali Zida alitoa hotuba yake katika runinga usiku kucha ili kutangaza kwamba anachukua mamlaka.
Hatua hiyo inaonekana kutofautiana na ile ya mkuu wa jeshi Jenerali Honore Traore ambaye alijitangaza kuwa kiongozi mpya mda mfupi baada ya kujiuzulu kwa Campaore.
Hatahivyo Sahihi ya Jenerali Honore Traore ilikuwa katika taarifa iliosomwa na Luteni kanali Issac Zida ambaye inadaiwa alichaguliwa na wakuu wote wa jeshi kuongoza.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment