Utafiti mpya umewaunga mkono wanawake wazee walio na wapenzi vijana.
Utafiti huo unasema kwamba wanawake wazee wanaotaka kupata watoto ni sharti watafute vijana wadogo.
Huku tafiti nyengine zikishindwa kubaini iwapo wanaume hufikia miaka ya kushindwa kuzaa,utafiti huu mpya kutoka Chuo kikuu cha Mc Gill nchini Canada umegundua kwamba ni vigumu kwa wanawake wazee kupata watoto na wanaume wa rika lao.
Utafiti huo unasema kuwa ijapokuwa wanaume hawana kiwango cha mwisho cha kutafuta watoto,fursa hiyo hupotea kila miaka inavyozidi.
Wakati unapotafuta watoto basi umri wa mwanamume ni muhimu tu kama ule wa mwanamke.
Utafiti huo uliwahoji takriban wanawake 631 walio na umri kati ya 40 na 46 pamoja na wapenzi wao walio na umri kati ya 25 na 70.
Wanawake hao baadaye waligawanywa katika makundi mawili kulingana na iwapo ni wazazi au la.
Watafiti hao wamebaini kwamba wanaume walio na miaka 43 na kuendelea uwezo wao wa kupata watoto uko chini ikilinganishwa na wale wa chini ya umri huo.
Utafiti huo pia umebaini kwamba wanawake wengi huanza kukosa kushika mimba wakiwa na miaka 40 huku wanaume nao wakianza kubahatisha wafikapo miaka 43.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment