Rais wa Zambia, Guy Scott
Waziri wa ulinzi nchini Zambia amesema kuwa Rais mpya wa mpito Guy Scott amemfukuza kwenye nafasi yake.
Edgar Lugu amesema Scott amevunja mwiko kumtimua kwenye nafasi yake akiwa Katibu Mkuu wa chama tawala cha Patriot Front wakati huu kabla ya Mazishi ya Marehemu Michael Sata.
Hivi sasa Scott anakaimu nafasi ya urais,akiwa Rais wa kwanza mweupe, baada ya kifo cha Michael Sata.
Kundi dogo la watu liliandamana mjini Lusaka kupinga uamuzi wa Scott.
Kuteuliwa kwa Scott kunatokana na muongozo wa Katiba ya nchi hiyo inayotaka Makamu wa Rais nafasi aliyohudumu tangu mwaka 2011, kuchukua majukumu ya Raisi mpaka uchaguzi utakapofanyika ndani ya siku 90.
Hata hivyo Scott hana vigezo vya kuwania nafasi ya urais kwa kuwa Katiba haimruhusu kwa kuwa wazazi wake hawakuzaliwa nchini Zambia.
CREDIT: BBC/SWAHILI
No comments:
Post a Comment