Wanasiasa, Maafisa wa kijeshi na Wanadiplomasia wa Ulaya wameitaka NATO kuongeza jitihada zaidi kusaidia mapambano dhidi ya ebola Afrika Magharibi.
Ugonjwa huu umeua watu takriban 5,000.Mtandao wa uongozi wa Ulaya ulituma barua juma lililopita kwa katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg wakimtaka kupeleka jeshi lake kwa ajili ya kusimamia miundombinu ili kuratibu mchakato wa mapambano dhidi ya ebola.
Wakati hayo yakijiri Rais wa Guinea Alpha Conde, akizungumza na BBC amekosoa nchi nyingine za Afrika magharibi akisema kuwa amesikitishwa na namna nchi jirani na wanachama wenzie wa ECOWAS na kitendo chao cha kufunga mipaka ya nchi zao inayopakana na Guinea.
Hata hivyo Conde amesema anaunga mkono jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na jumuia ya kimataifa kupambana na ebola lakini ametahadharisha kuwa ugonjwa huo unazorotesha uchumi wa Guinea.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment