Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Saturday, 1 November 2014
MEGAWATI 2,780 ZA UMEME KUZALISHWA TANZANIA IFIKAPO 2025
Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
Arusha: MAKAMU wa Rais, Dk Mohammed Bilal amesema serikali ya Tanzania inatarajia kuzalisha umeme Megawati 2,780 ikilinganishwa na sasa ipo megawati 1,478, huku usambazaji utaongezeka kwa asilimia 50 kutoka asilimia 36 ifikapo mwaka 2025.
Aliyasema hayo jana Jijini Arusha, wakati akifungua mkutano wa Nishati Mbadala wa Joto Ardhi (Jadilifu), ulioshirikisha wataalamu zaidi ya 400 toka nchi mbalimbali Duniani.
Alisema ukuaji wa utumiaji umeme umekua kwa asilimia 14 toka asilimia 6, huku wakitarajia kuongeza ukuaji huo na kufikia asilimia 36.
Dk. Bilal alisema kuwa serikali ya Tanzania kwa kuongeza nguvu katika sekta ya umeme kumesaidia kuongeza ukuaji wa uchumi.
“Hapa tukizalisha nishati hii ya joto ardhi tutaongeza wawekezaji wa kimataifa watakaokuja kuwekeza sekta ya viwanda, kilimo,biashara na Miundo mbinu,” alisema.
Naye Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Steven Maselle, alisema ili Tanzania iweze kuwa kama nchi zilizoendelea duniani, inapaswa kuzalisha umeme Megawati 10,000.
“Hali ya utulivu wa nishati ya umeme itakuwa ni nzuri kama tutazalisha Megawati hizo, lakini zikiendelea kubaki kama zilivyo nchi haiwezi kupata maendeleo ya haraka, hususani sekta ya viwanda na kilimo,” alisema.
Masele alisema Nishati ya Joto ardhi utasaidia kuongezeka nishati ya umeme nchini, kwani chanzo hicho cha kudumu na kinatoka kwenye Bonde la Ufa na hakiwezi kufa.
Alitoa wito kwa watanzania kuwa watulivu na kuachia wataalamu kufanya utafiti utakaowezesha kuzalisha kwa umeme mwingi kupitia vyanzo mbalimbali kikiwemo cha joto ardhi.
Pia alisema Tanzania kuna vyanzo vya joto ardhi zaidi ya 50 vinavyoweza kuzalisha umeme megawati 5000, hivyo chanzo hicho kitakuwa kichocheo kikubwa cha kukua kwa uchumi wan chi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment