Jopo la Umoja wa Mataifa la wataalamu wa sayansi ya hali ya hewa, limeonya leo kuwa mabadiliko makubwa yanatokea katika hali ya hewa duniani na haitawezekana kurejesha hali ya zamani iwapo gesi zinazozidisha joto duniani, hazitaondoshwa kabisa ufikapo mwisho wa karne.
Ripoti iliyokubaliwa kwenye mkutano mjini Copenhagen, imechapishwa leo.
Dakta Peter Gleick ni mwana-sayansi wa mabadiliko ya hali ya hewa ambaye ameiona ripoti hiyo.
Aliiambia BBC, ushahidi wa kisayansi ni mzito sasa, kuwa binaadamu ndiye chanzo cha mabadiliko ya hali ya hewa:
"Bila ya shaka watu wasioamini kuwa wanaadamu ndio wanasababisha mabadiliko ya hali ya hewa, hawataki kusikiliza sayansi.
Kuna masuala magumu ya kisiasa yanahitaji kuamuliwa, lakini siyo ya kisayansi tena.
Ushahidi katika sayansi ni thabiti - kwamba hali ya hewa inabadilika; kwamba wanaadamu ndio wanayosababisha hayo.
Na kwamba ikiwa hatuchukui hatua sasa, basi totaona matokeo makubwa na hasara itakuwa kubwa kwa watu na dunia yenyewe."
Na Waziri wa Mashauri ya nchi za Nje wa Marekani, John Kerry, alisema wale wanaodharau sayansi kuhusu hali ya hewa iliomo kwenye ripoti hiyo, wanahatarisha maisha yetu, watoto na wajukuu wetu.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment