HUWEZI kuamini kwamba tunautumia muda mwingi kwa shughuli zetu za kidunia kiasi kwamba tunamsahau Mungu. Hata tunapopata nafasi kidogo ya kwenda kanisani au msikitini, wengine huwa wanaona kero hivyo kufanya ibada kuwa kama mazowea tu bila kunuia.
Lakini kuna wahubiri wengine na watoa mawaidha huwa wanajisahau. Wanatumia muda mwingi kueleza mambo mengi kwa wakati mmoja na kuwafanya watu wasahau yaliyotangulia kusemwa. Kwa vile siyo busara kuondoka ibadani wakati wa mahubiri, wengine huamua kuketi lakini mawazo yao yakiwa mbali.
Sasa sikiliza kisa hiki cha mhubiri aliyetumia muda mwingi kuzungumza mambo mengi kiasi cha kumchanganya mmoja wa waumini wake. Alipomaliza akawauliza waumini ambao walikuwa kimya wakati akihubiri:
"Nani anataka kwenda Mbinguni?" (Watu wengi wakanyoosha mikono huku wakipiga vigelegele).
Akauliza tena: "Nani anataka kwenda motoni?" hakuna aliyenyoosha mkono.
Lakini kulikuwa na muumini huyu mmoja ambaye muda wote wa mahubiri alikuwa ametulia tuli 'akisikiliza' kwa makini. Ajabu ni kwamba, hakunyoosha mkono mahali popote katika maswali yale mawili yaliyoulizwa.
Mhubiri akamsogelea akiwa na kipaza sauti akitaka kujua kama huyo bwana amemwelewa ama alikuwa na mawazo gani.
Akamuuliza: "Mpendwa, hukunyoosha mkono kati ya wanaotaka kwenda Mbinguni, wala hukunyoosha mkono kati ya wanaotaka kwenda motoni. Sasa wewe unataka kwenda wapi?"
Muumini: NATAKA KWENDA NYUMBANI, EBOH!
No comments:
Post a Comment