Shirika la kutetea haki za Binadamu la Amnesty International limeilaumu Serikali ya Ujerumani kwa madaia inakiuka sheria za kimataifa kwa kuwarejesha wakimbizi wa Somalia katika eneo ambalo linashikiliwa na wapiganaji wa kundi la Al Shabab.
Amnesty imesema kuwa waomba hifadhi kutoka Somalia ambao nao pia wamerejeshwa wanaweza kukabiliwa na hukumu za vifo nchini humo hali ambayo shirika hilo limeiomba Ujerumani kubadili sera zake.
Hata hivyo idara ya uhamiaji ya Ujerumani imesema kila ombi la waomba hifadhi lilipitiwa kwa makini na kwamba wengi wao walipendekeza kurejea nchini kwa Somali na kudaia kuwa hawajawalazimisha kurejea kwa nguvu.
Mwezi mei mwaka huu Umoja wa mataifa ulipendekeza nchi zinazo wahifadhi wakimbizi wa Somalia kutowarejesha nchini kutokana na machafuko na hatari kwa maisha yao.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment