Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 6 August 2015

WANACHAMA WAVAMIA OFISI ZA CUF

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof.Ibrahim Lipumba, katika moja ya mikutano ya chama hicho. Jana alizuiwa na wanachama wake kuendesha mkutano na waandishi wa habari wakitaka aeleze tetesi kwamba alitaka kujiuzulu uenyekiti. 

Na Sauli Giliard
 Dar es Salaam. WANACHAMA wa Chama cha Wananchi (CUF) wamevamia makao makuu ya chama hicho jana asubuhi na kusababisha kikao cha mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba na wanahabari kuhairishwa.
Mkutano wa mwenyekiti huyo ulikuwa ufanyike jana saa nne asubuhi makao makuu ya Cuf yaliyopo Buguruni, Dar es Salaam lakini hadi saa tano, mwenyekiti alikuwa kwenye kikao cha ndani na “wazee wa chama” waliokuwa wanataka ufafanuzi kwa baadhi ya mambo.
“Wazee wanataka ufafanuzi kwa baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na taarifa zilizoenea kuwa amejiuzulu,” amesema Magdalene Sakaya, Naibu Katibu Mkuu Bara amewaamabia wanahabari.
Hata hivyo, wananchama waliokuwa nje wakati mwenyekiti Lipumba akiendelea na kikao cha ndani cha chama hicho walionyesha kushtushwa na taarifa zilizochapishwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kuwa Profesa Lipumba ameachana na siasa za chama hicho.
Wasiwasi huo uliongezeka jana mara baada ya mtaalamu huyo wa uchumi kutoonekana wakati wa kumtangaza Edward Lowassa kuwania urais kupitia Chadema, moja ya chama kinachounda Ukawa huku Juma Duni Haji akipitishwa kama mgombea mwenza.
CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment