Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 31 August 2015

HALMASHAURI NZEGA YAJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA YA MAJI

Mhandisi wa maji Halmasauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora Mariam Majala akitoa ufafanuzi. Picha na Hastin Liumba.

Na Hastin Liumba, NzegaSERIKALI ya Tanzania ahadi yake kubwa siku zote inatekelezwa chini ya Ilani ni pamoja na suala zima la upatikanaji wa huduma za msingi kwenye maisha ya kila Mtanzania.
Yapo matatizo ambayo yanapelekea jamii kushindwa kupata mahitaji yake ya msingi huku jamii hizo zikiishia kuitwa masikini hali ambayo wakati mwingine inazaa matunda hata kwa vizazi vijavyo.

Matatizo hayo ni pamoja na huduma za msingi kama Maji, Afya, Elimu pamoja na masuala ya utawala bora ambayo yana uhitaji mkubwa hasa kwa baadhi ya maeneo.

Hata hivyo utekelezaji wa miradi hiyo ambayo ina matatizo wakati mwingine inaweza kufanyika lakini pia isifanyike kulingana na msukumo wa viongozi walio ndani ya halmashauri husika.

Mamlaka ya maji safi na maji taka wilaya ya Nzega mkoani Tabora (NZEWASA) imejipanga kuhakikisha huduma ya upatikanaji wa maji safi inaboreka na wananchi wananufaika na huduma hiyo kwa ufasaha.

Mariamu Majala Mhandisi wa maji wilaya ya Nzega mkoani Tabora anazunguzia hali ya upatikanaji wa maji,mipango ya baadaye ya sasa na changamoto zake kwenye utekelezaji wa miradi ya maji wilayani humo wakati wa mahojiano na mwandishi wa makala hii.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nzega Abrahaman Mndeme, Majala anasema hadi sasa kama halmashauri wana miradi ambayo wameanza kuitekeleza katika kipindi cha mwaka 2005 inayojulikana kama Programu ya maendeleo sekta ya maji WSDP 2006.

Anaongeza mradi huo umelenga vijiji 10 kila wilaya kwa nchi nzima,ambapo wilaya ya Nzega vijiji tayari mradi unatekelezwa.

Majala alitaja vijiji hivyo 10 kuwa ni Uhemeli, Itobo, Nata, Sigili, Nkiniziwa, Upungu, Ikindwa, Nawa, Mahene na Uhondo.

Alisema vijiji ambavyo viliwezeshwa utafutiwaji wa vyanzo vya maji ili uchimbaji wa maji vijijini uanze kati ya vijiji 10 ni vijiji saba vilipata maji ya kutosha na kujengewa miundombinu ya maji kama Tanki,Gati na kuunganishiwa na Bomba.

Hata hivyo mhandisi huyo anabainisha kuwa katika vijiji  vilivyokosa maji kabisa ni Nkiniziwa na Upungu kutokana na ukame uliopo kwenye maeneo hayo.

Alisema kijiji cha Sigili kilipata maji kidogo na kama halmashauri walipeleka Pampu ya mikono katika kipindi cha mwaka 2009/2010 ambapo gharama za miradi kwa kipindi hiki ni sh milioni 269,270,600.

Mhandisi Majala anasema katika kipindi cha mwaka 2012/2013 halmashauri Nzega kuingia mikataba ya wazabuni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji katika vijiji sita na gharama zake ni sh Bilioni 1.4.

Alitaja vijiji hivyo kuwa ni Nawa, Buhondo,Mahene,Ikindwa,Sigili, vijiji ambavyo vitaunganishwa na mabomba wakati kijiji cha Uhemeli kitawekewa Pampu ambapo hadi sasa huduma ya maji imekamilika.

Alisema katika mradi huo jumla ya wanufaika 40,500 wanapata huduma hiyo.

Aidha anaongeza katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2013/2014 halmashuri iliingia mikataba ya wakandarasi kwa ajili ya ujjenzi wa miundombinu ya maji kwa vijiji vitatu vya Nata,Itobo ambapo miradi yote kwa sasa imekamilika wakati mradi huo kwa kijiji cha Nkiniziwa upo kwenye hatua ya ukamilishaji.

Alisema katika kipindi cha mwaka fedha wa 2013/2014 gharama za kutekeleza miradi hiyo ni Shs. 2,170,517,594.

Anasema katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2014/2015 jumla ya visima 14 vilipangwa kuchimbwa kwa kiasi cha sh 420 katika vijiji vya Upima,Isunha,Shigamba,Usagali,Silimuka 2,Utwingu, Nhundo,Bulende,Utwigu,Kitwengwe,Upungu,Wela na Sigela.

aidha alisema ujenzi wa miundombinu mipya ya maji katika vijiji vya Upungu, Silimuka, Mbangwa,Ngukumo na Sigili taratibu za ujenzi zinafanyika na jumla ya sh milioni 700 zimpokelewa,na ukarabati wa mtandao wa maji ya bomba Kampala,  Zogolo, Sojo na Bukene jumla ya sh milioni 300 zimetengwa.
Vyombo vya wananchi vimeundwa.

Mhandisi Majala anasema ili kushirikisha jamii na wananhi kwa ujumla vyombo huru vimeundwa na wananchi hao kwa ajli ya ufuatiliaji wa matumizi ya maji.

Alisema vyombo vyote vilipata mafunzo kwa ajili ya kujiendesha katika miradi hiyo ya maji.

Changamoto za miradi

Anazungumzia changamoto za utekelezaji wa miradi ya maji ni pamoja na bado kuna mwamko mdogo kwa upande wa uchangiaji miradi ya maji na huduma za maji.

Anataja changamoto nyingine ni usimamizi duni wa miradi ya maji kutokana na hali halisi wajumbe wachaguliwa katika vyombo huruvilivyoundwa kuendesha,kusimamia miradi hiyo.

Aidha anaeleza upungufu wa watumishi wa idara ya maji nalo ni tatizoambapo mahitaji halisi ni watumishi 28 kwa sasa wapo 6 tu,huku bado kuna uharibifu wa miundombinu ya maji unaofanywa na baadhi ya watu wanaiba na kuuza kama chuma chakavu.

Aidha anasema bado kuna uhaba wa fedha za ufuatiliaji wa miradi ya maji toka serikali kuu nalo ni tatizo kwao.

Mikakati na malengo yake

Mhandisi Majala anasema malengo na mikakati waliyojiwekea kama halmashauri kutoa elimu tosha jamii kusimamia miradi ya maji ambapo elimu hiyo itakuwa endelevuo.

Aidha aliishauri serikali kuu kupanua wigo wa ajira ili kuwepo na watu watakaosadia usimamiazi wa miradi ya maji ya vijiji na Kata.

Aidha alishauri wizara ya maji ifanye kama wizara nyingine kwa kuweka utaratibu wa kutoa ruhusa ya kuajiri watumishi eneo la usimamizi.

Hata aliishauri pia serikali kuu kutenga fedha na kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya mafunzo na ufuatiliaji miradi ya maji ya vijiji na kata.
hastinliumba@gmail.com-0788390788

No comments:

Post a Comment