Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 25 August 2015

PINGAMIZI DHIDI YA PROFESA MAGHEMBE LATUPWA

Waziri wa Maji ambae pia ni Mbunge wa Mwanga
Waziri wa Maji ambae pia ni Mbunge wa Mwanga, Profesa Jumanne Maghembe. 

Na Daniel Mjema
Mwanga. Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Mwanga ametupilia mbali pingamizi zilizowekwa na mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema, Henry Kileo dhidi ya wagombea wenzake wawili.
Kileo aliweka pingamizi dhidi ya Waziri wa Maji na mbunge anayemaliza muda wake, Profesa Jumanne Maghembe (CCM) na Mgombea wa NCCR-Mageuzi, Youngsaviour Msuya ambaye ni wakili kitaaluma.
Kwa mujibu wa Kileo, wagombea hao hawakuwa wamewasilisha tamko rasmi la kisheria lililotolewa mbele ya hakimu mkazi wa Wilaya ya Mwanga na pia, hawakuwa wamedhaminiwa na vyama vyao.
Kileo alidai mihuri iliyogongwa katika fomu zao ni ya katibu wa wilaya badala ya ofisi ya wilaya. Pia, alidai kuwa picha ya Profesa Maghembe haikupigwa ndani ya miezi mitatu.
Hata hivyo, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Jamhuri William ametupilia mbali sababu hizo akidai kuwa kumbukumbu alizonazo ofisini kwake wagombea hao wamedhaminiwa na vyama vyao.
Alisema hatua ya Msuya kutoa tamko mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Moshi haimuondolei sifa ya kuteuliwa mgombea na pia, haoni tatizo kwa Profesa Maghembe kula kiapa Mahakama ya Mwanzo. “Masuala yanayohusu mihuri ya chama inategemea na muundo wa uongozi na utendaji katika chama husika. Hakuna kosa kwa katibu wa wilaya kugonga muhuri wake,” alisema msimamizi huyo.
William alifafanua kuwa suala la umri wa picha ya Profesa Maghembe halina uthibitisho na kwamba, malipo ya risiti ya tamko rasmi siyo mojawapo ya sharti la uteuzi wa mgombea ubunge.
Baada ya kutupwa kwa pingamizi lake, Kileo aliliambia gazeti hili jana kuwa atakata rufaa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) akipinga uamuzi huo wa msimamizi kuwa haukutenda haki.
Kileo alisema mathalani katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwaka jana, baadhi ya wagombea wa Chadema walienguliwa baada ya fomu zao kugongwa muhuri na katibu wa wilaya.
CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment