Chelsea wanasajili ushindi muhimu wa mabao 3-2 dhidi ya West Brom ugenini.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na kiungo mgeni kutoka Uhispania Pedro katika dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza.
Hii ndiyo iliyokuwa mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na 'the Blues'' katikati ya juma hili.
West Brom watajilaumu wenyewe baada yao kupoteza fursa ya kuilaza Chelsea mapema walipopoteza penalti.
James Morrison alipiga mkwaju hafifu na kipa Courtois hakufanya masihara nao.
Courtois ambaye alikuwa anacheza mechi yake ya kwanza tangu aoneshwe kadi nyekundu majuma mawili yaliyiopita alikuwa na kila sababu ya kutabasamu na kumfanya kocha Mourinho amsamehe kwa makosa yaliyopelekea yeye kutimuliwa.
Hata hivyo Diego Costa aliongezea matumaini ya the Blues kusahau kichapo walichopata majuzi alipofanya mambo kuwa mabao mawili kwa nunge kunako dakika ya 30.
West Brom waliendelea kuuliza safu ya ulinzi ya Chelsea maswali na wakapata majibu kunako dakika ya 35 Morrison aliporekebisha makosa yake na kuifungia West Brom bao lao la kwanza.
César Azpilicueta alimhakikishia Mourinho alama zote tatu muhimu kwa bao lake la dakika ya 42.
James Morrison aliendelea kuwa mwiba katika safu ya ulinzi ya Chelsea .
Gonga gonga yake ilisababisha bao la pili kwa mkwaju wa kichwa.
West Brom waliendelea kufanya mashambulizi na shinikizo lao likasababisha Kiungo wa Chelsea John Terry kuoneshwa kadi nyekundu kwa kumburura Salomón Rondón.
Mwisho wa kuishia The Blues wanarejea darajani wakiwa wametia kibindoni alama tatu muhimu.
Chelsea wanasajili ushindi muhimu dhidi ya West Brom ugenini.
Mpira umekwisha.
90:02
West Brom 2-3 Chelsea ''
John Obi Mikel anaingia uwanjani kuchukua pahala pa Pedro
83:02
Freekick kwa upande wa Chelsea (Pedro)
82:13 West Brom 2-3 Chelsea
West Bromwich Albion wanajipatia kona Branislav Ivanovic.
70:13
Gary Cahill akiwa amevalia barakoa baada ya kujeruhiwa pua
Je uamuzi wa refarii Mark Clattenburg kutoa kadi nyekundu umekurithisha ?
65:28 West Bromwich Albion 1- 3 Chelsea
GOOOOOOOL
James Morrison anafungia West Brom bao la pili kwa kichwa
58:34West Brom 2-3 Chelsea
West Bromwich Albion 1- 3 Chelsea
53:21 John Terry (Chelsea) anaoneshwa kadi nyekundu
50:34
West Bromwich Albion 1- 3 Chelsea
46:41
Kona kuelekea lango la Chelsea
45:00 Pedro anaunawa mpira
West Bromwich Albion 1, Chelsea 3.
Kipindi cha pili kimeanza
Kipindi cha kwanza kimekamilika hapa The Hawthorns
Matokeo ni West Bromwich Albion 1- 3 Chelsea
45:00
West Bromwich Albion 1- 3 Chelsea
41:40 Goal scored
Goooooooooool!
West Bromwich Albion 1- 3 Chelsea
César Azpilicueta
30:00
West Bromwich Albion 0, Chelsea 2
29:01
GOOOOOOL Diego Costa anaifungia chelsea bao la pili West Bromwich Albion 0, Chelsea 2 ''
24:01
West Brom 0-1 Chelsea
19:30
GOOOOOOOOAL
Pedroooooo
Pedro akifungua akaunti yake Chelsea
West Brom 0-1 Chelsea
17:45 West Brom 0-0 Chelsea
Freekick kuelekea lango la Chelsea
Callum McManaman (West Bromwich Albion) anachezewa visivyo
16:11
Nemanja Matic (Chelsea) anaoneshwa kadi ya njano
12:35 LOOOOOOO
Penalti inaokolewa hapa
Amini usiamini James Morrison wa West Bromwich Albion anapiga mpira hafifu na kipa nambari moja Courtois anathibitisha kwanini yeye ndiye anayepewa majukumu langoni
12:27 Penalti kuelekea lango la Chelsea
Nemanja Matic anacheza visivyo
5:03 West Brom 0-0 Chelsea
Diego Costa anafanya mashambulizi ya mapema mbele ya lango la wenyeji wao
3:21
West Brom v Chelsea
Salomón Rondón wa West Bromwich Albion anamjaribu kipa wa Chelsea Courtios
Mechi imeanza kwa kishindo
West Bromwich Albion
13 Myhill 25 Dawson 23 McAuley 03 Olsson 11 Brunt 24 Fletcher 05 Yacob 19 McManaman 14 McClean 07 Morrison 33 Rondón
Wachezaji wa akiba
04 Chester 06 Lescott 08 Gardner 10 Anichebe 17 Lambert 31 Gnabry 38 Rose
Kikosi cha Chelsea;
13 Courtois 02 Ivanovic 26 Terry 05 Zouma 28 Azpilicueta 04 Fàbregas 21 Matic 17 Pedro 22 Willian 10 Hazard 19 Diego Costa
Wachezaji wa akiba
01 Begovic 09 Falcao 12 Mikel 14 Traore 18 Remy 24 Cahill 36 Loftus-Cheek
Victor Moses na Oscar, hawatakuwa uwanjani baada ya kuripotiwa kujeruhiwa mazoezini
Kocha Jose Mourinho anajivunia kiungo mpya Pedro
Chelsea wanahitaji ushindi kwa udi na uvumba ilikufufua kampeini yao msimu huu.
Bila shaka Mourinho angependa kugonga vichwa vya Habari kwa kushinda wala sio kutofautiana na kitengo cha utabibu
Karibu katika matangazo ya moja kwa moja kati ya West Brom na Chelsea.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment