Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 25 August 2015

MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU YAFANYIKA DAR ES SALAAM

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini hawapo pichani wakati akifunga mafunzo ya wiki nane ya ujasiriamali kwa wanafunzi hao mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yaliendeshwa chini ya mpango wa Cambridge Development Initiative (CDI) ili kuimarisha mafunzo ya maswala ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini. CDI ni mpango ulioasisiwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cambridge cha nchini uingereza. Kulia ni Rais wa CDI, Ravi Solanki.
2
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa (katikati) akikabidhi hundi ya dola 3000 kwa wanafunzi wawili kutoka chuo kikuu cha Ardhi walioibuka washindi kwa wazo bora la biashara baada ya mafunzo ya wiki nane ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na NEEC kwa ushirikiano na mpango wa Cambridge Development Initiative (CDI) unaoendeshwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cambridge cha nchini Uingereza. Wengine ni Moses Mtei, mshindi (kushoto); Mkurugenzi wa Ujasiriamali CDI, Bi. Georgia Ware (kulia); na Joel Kissava pia mshindi toka Chuo kikuu Ardhi (wapili kulia). Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
3
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa (wa pili kushoto) akikabidhi hundi ya dola 3000 kwa mmoja wa wanafunzi walioibuka washindi kwa wazo bora la biashara baada ya mafunzo ya wiki nane ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na NEEC kwa ushirikiano na mpango wa Cambridge Development Initiative (CDI) unaoendeshwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cambridge cha nchini Uingereza. Wengine ni Bhoke Nyaisaba toka UDSM, mshindi (kulia); Mkurugenzi wa Ujasiriamali CDI, Bi. Georgia Ware (wa pili kulia); na mwanafunzi toka UDSM, Vivian Mushi (kushoto). Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment