Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 5 August 2015

KAPUYA ANUSURIKA, DK. KAFUMU ASHINDA

Prof. Juma Kapuya

Na Hastin Liumba, KaliuaWAKATI  matokeo ya kura ya maoni  yakiendelea kutolewa mkoani Tabora kutoka katika majimbo kadhaa mbunge za wamani wa jimbo la Kaliua Profesa Juma Kapuya ameshinda kwa kura nyingi.
Kapuya alipita ushindi huo baada ya kubwanga kijana Imani Matabula kwa kura zaidi ya 6,000 wakati ambapo Profesa Kapuya alipata kura 9,204.
Akitangaza jimbo jipya la Ulyankulu Katibu wa CCM wilaya ya Kaliua Neema Adamu alisema kwamba katika jimbo hilo aliyeongoza ni John Kadutu aliyepata kura 14,512 na kufuatiwa na  Dkt Siden Msonde 2,194 Edward Mdaki 797 na  Saul Kauzu 561.
Akutangaza matokeo hayo kaimu katibu wa wilaya hiyo na katibu wa vijana mkoa wa Tabora Mariam Amri alisema kwamba katika jimbo la Manonga mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Tabora Seif Hamisi Gulamali alimshinda mweyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwa kupata kura 8,091 na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Abubakari Shabani kura 2,865.
Aidha katika jimbo la Sikonge matokeo yake bado kutolewa kutokana na kurudiwa uchaguzi katika kata mbili ambazo kura zake zilikuwa na utata na mara baada ya kukamilika zitatolewa kwa vyombo vya habari ambapo taarifa za awali zinaonyesha mbunge Said Nkumba ameanguka katika baadhi ta vituo huku Rajab Kakunda akiongoza vituo vingi.

DK. KAFUMU ASHINDA KURA ZA MAONI IGUNGA
ALIYEKUWA mbunge wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora Dk. Dalali Peter Kafumu ameshinda katika uchaguzi kura za maoni  dhidi ya wagombea wenzake watano.
Kafumu ambaye ameongoza kwa kupata kura  7,037  huku akifatiwa  na Nicolaus  Ngassa 2,378 Jafali Omary 1,945 Nathanile Mboje  991 Hamad Hamdani 410  Angela milembe 184 .
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa uchaguzi amesema Jimbo la Igunga Abdalah Kazwika alisema lina kata 15 ambapo wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  ndio waliopiga kura za maoni .
Naye Dk, Kafumu  baada ya kutangazwa matokeo hayo alisema kwa sasa kinachoendelea  ni kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kuweza kukipatia ushindi chama cha mapinduzi katika uchaguzi ujao wa oktoba 25, 2015.
Nao  baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi ccm katika jimbo la Igunga wamewataka wagombea wote walioshindwa katika kura za maoni kuunganisha nguvu zao kwa pamoja ili kuweza kukipatia ushindi chama hicho.

No comments:

Post a Comment