Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 31 October 2014

BAADA YA MAPINDUZI, JENERALI TRAORE AJITANGAZA RAIS BURKINA FASO

Jenerali Honore Traore mkuu wa jeshi la Burkina Faso aliyejitangaza rais mpya wa nchi hiyo
Mkuu wa Jeshi la Burkina Faso Jenerali Honore Traore sasa amejitangaza kuwa rais baada ya aliyekuwa rais wa Burkina Faso Blaise Compaore kutangaza kujiuzulu.

RAIS COMPAORE AJIUZULU, JESHI LASHIKA HATAMU BURKINA FASO

Bwana Compoare amejiuzulu
Aliyekuwa rais wa Burkina Faso Bwana Compaore sasa ametaka uchaguzi mpya wa urais ufanyike baada ya siku 90.

LOWASSA, MAKAMBA 'WAGONGANA' KANISANI

January Makamba na Edward Lowassa 
Mahenge. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba wamewaomba viongozi wa dini kuwasamehe viongozi wa Serikali waliokwaruzana nao wakati wa mchakato wa Katiba na kuliombea Taifa lipate viongozi wenye hekima na uwezo katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

WABUNGE TISA WAJIUZULU KUMPINGA SHY-ROSE BHANJI

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Shy-Rose Bhanji. Picha na Maktaba 
Na Neville Meena, Mwananchi
Dar es Salaam. Mgogoro ndani ya Bunge la Afrika Mashariki (Eala) umechukua sura mpya baada ya wabunge tisa, wakiwamo makamishna watano na wenyeviti wanne wa kamati za Bunge hilo, kuwasilisha barua za kujiuzulu nafasi zao hizo, ikiwa ni matokeo ya sakata linalomhusisha mbunge mwenzao kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji.

SERIKALI ISIKWEPE KULIPA MALIMBIKIZO YA MADENI MSD KUOKOA MAISHA YA WATANZANIA!


Taarifa kwa Vyombo Vya Habari, 30 Octoba 2014

Serikali isikwepe kulipa malimbikizo ya madeni MSD kuokoa maisha ya Watanzania!

Sikika imesikitishwa na tamko lililotolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, kuhusiana na kushindwa kwa vituo vya huduma za afya kununua dawa MSD kutokana na kuongezeka kwa deni. Ni wazi kuwa waziri hajalipa tatizo hili uzito unaotakiwa na kutambua kuwa baadhi ya wagonjwa wanaweza kupoteza maisha kutokana na tatizo hili.

POLISI ASHIKILIWA KWA KUMKATA MFANYAKAZI WAKE VIDOLE VINNE KWA PANGA KWA MADAI YA KUMWIBIA DEKI YA VIDEO

Ni kidole gumba tu kilicho nusurika kukatwa nacho ilikuwa ni kama bahatikusalia kwani kilikwanyuliwa huku vingine vinne vikifyekwa na panga mkono wa kulia wa Steven Magessa.

JESHI la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia askari wake WP Fatuma wa Kituo cha Polisi Igogo wilayani Nyamagana kwa kosa la kumjeruhi mtumishi wake wa ndani kwa mkumkata vidole vyake vinne vya mkono wa kulia kwa panga, akimtuhumu kumwibia Deki ya Video nyumbani kwake. 

TAARIFA YA UKAGUZI MAALUM WA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW (UKAGUZI WA IPTL)


TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA YA UKAGUZI MAALUM WA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW (UKAGUZI WA IPTL)


Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inapenda kuujulisha Umma kuwa Ukaguzi Maalum wa akaunti ya Tegeta Escrow ambao unafahamika kama Ukaguzi wa IPTL unaendelea na unaongozwa na Hadidu za Rejea (ToR) zilizotolewa na kisha kuridhiwa na Ofisi ya Bunge na Wizara ya Nishati na Madini.

MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA YA HUDUMA KWA JAMII AMTEMBELEA WAZIRI CHIKAWE OFISINI KWAKE DAR LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii ambaye pia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Shaaban Lila, wakati Jaji huyo alimpomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kujadiliana masuala mbalimbali ya Adhabu Mbadala wa Kifungo.  Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.    

UN YAOKOA MAISHA YA WATOTO 3,000 ZANZIBAR

DSC_0152
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari wa Zanzibar kwenye ofisi ndogo za mashirika ya Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar kuhusiana na mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na kushoto ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu.

MAKOCHA 35 KUSHIRIKI KOZI YA LESENI C YA CAF


Na Mwandishi Wetu
Makocha 35 wameteuliwa kushiriki kozi ya ukocha ya Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itakayofanyika mjini Morogoro kuanzia Novemba 5 hadi 19 mwaka huu.

CCM YATOA PONGEZI KWA FRELIMO KWA USHINDI KATIKA UCHAGUZI MSUMBIJI

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti,makao makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es Salaam.

UFISADI WA BILIONI 3.2/- WABAINIKA TWIGA BANKCORP


Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe

Na Isaya Kisimbilu
Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeibua ufisadi wa zaidi ya Sh. bilioni 3.2 katika Benki ya Twiga Bancorp, kutokana na wizi unaodaiwa kufanywa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo ya fedha kwa muda mrefu.

KIVUMBI CHA LIGI KUU ENGLAND KESHO, LIVERPOOL WAKO UGENINI KWA NEWCASTLE

Golikipa Simon Mignolet wa timu ya Liverpool ashindwa kuupangua mpira.
Kitimtim cha ligi kuu ya England kitaendelea tena kesho wakati ambapo mashabiki wa soka nchini humo na duniani kote watapata nafasi ya kuzishuhudia timu zao zikitafuta pointi tatu muhimu.

RAIS COMPAORE WA BURKINA FASO ASEMA ATAJIUZULU BAADA YA MIEZI 12

Rais Blaise Compaore
Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso amesema atajiuzulu baada ya miezi 12 ya serikali ya mpito.

SKYLIGHT BAND INAKUKARIBISHA USIKU WA LEO THAI VILLAGE KWA BURUDANI YA KIPEKEE KABISA!

DSC_0159
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku akisindikizwa na waimbaji wenzake kutoka kushoto ni Digna Mbepera, Joniko Flower a.k.a Baba lao, Sony Masamba pamoja na Sam Mapenzi.

WAHUDUMU WA EBOLA WAONGEZEWA MOTISHA

Gavana wa jiji la New York Andrew Cuomo
Serikali ya Marekani imeongeza fedha kwa wafanyakazi wa sekta ya afya wanaowahudumia watu walio athiriwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola ,lengo ni kuwavutia manesi na madaktari wengi zaidi kwenda kutoa huduma katika nchi za Afrika Magharibi.

WAZIRI WA FEDHA -SAADA MKUYA AONGOZA UZINDUZI WA CHAPISHO KUU LA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI 2011-2012-TANZANIA BARA

 Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo uliofanyika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo asubuhi akihutubia.

TAZAMA VIDEO NAMNA AKINADADA WANAVYOPATA MATESO KWA AJILI YA KUTENGENEZA MAKALIO NA MATUMBO YAO!

Ukitaka uzuri lazima udhurike! Hakika wanawake wanapata mateso makubwa kwa ksingizio cha kutengeneza makalio, matumbo na matiti yao eti ili wawe na maumbo mazuri. Tazama mwenyewe upasuaji huu.

HII NDIYO HUKUMU YA MWIZI, INATISHA!

Wanadamu wanachukua sheria mikononi ama hukumu inatolewa duniani? Miye sielewi. Tazama namna maisha ya kijana huyu yanavyotoweka huku mwenyewe akiona pamoja na jitihada zake zote za kupigania uhai wake.

MWANDISHI WA AL-JAZEERA AKAMATWA MISRI

Nembo ya Kituo hicho
Mwanafunzi wa chuo kikuu nchini Misri ambaye hufanya kazi ya kupiga picha na uandishi wa runinga wa kituo cha Al- Jazeera amekamatwa na kuwekwa korokoroni.

TAARIFA ZISIZO ZA KWELI KUHUSU UTEUZI WA KONSELI WA HESHIMA JIMBO LA GUANDONG, CHINA


Hivi karibuni kumezuka taarifa za upotoshwaji zilizotolewa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Serikali ya Tanzania imemteua Bw. Salaah, Mkurugenzi wa Home Shopping Centre, (pichani ) kuwa Konseli wa Heshima (Honorary Consul) kwenye mji wa Guangzhou kwenye Jimbo la Guandong. 

PRESIDENT KHAMA APPOINTS CABINET 2014

President Seretse Khama Ian Khama

PRESIDENT KHAMA APPOINTS CABINET
The President, Lt Gen. Seretse Khama Ian Khama, has appointed members of cabinet as follows:

Thursday 30 October 2014

AMINI USIAMINI, JESHI LAPINDUA SERIKALI BURKINA FASO

Bunge la Burkina Faso limetekezwa moto
Amiri jeshi mkuu wa jeshi la Burkina Faso  Jenerali Honore Traore ametangazwa kuvunjwa kwa serikali na bunge la taifa.

TAARIFA YA TRA KUHUSU YATOKANAYO NA ZIARA YA UJUMBE WA IMF


HABARI KWA UMMA

Ujumbe wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Wahitimisha Ziara yake Tanzania

Ujumbe wa wataalamu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ukiongozwa na Bw. Hervé Joly ulitembelea Tanzania kuanzia tarehe 16 hadi tarehe 29 Oktoba 2014. Ujumbe wa IMF umefanya majadiliano ya tathmini ya kwanza ya Mpango wa Ushauri wa Sera za Uchumi (Policy Support Instrument -PSI) ulioidhinishwa na Bodi Tendaji ya IMF tarehe 16 Julai, 2014.

SERIKALI YASHAURIWA KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA FILAMU


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akiowaonyesha mabango ya filamu za Tanzania wageni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (hawapo pichani) walipotembelea ofisi za Bodi hiyo ili kujifunza namna ya Uendeshwaji wa Bodi ya Filamu jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw. Silyvester Sengerema.

Kutoka kushoto ni Afisa Mult Media kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (CA) Bi. Jacquline Kinyanjui, Afisa Mult Media kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya Bi. Mercy Tepla na Afisa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. George Charles wakisikiliza maelezo kutoka kwa uongozi wa Bodi ya Filamu Tanzania walipotembelea ofisi za Bodi hiyo jana jijini Dar es Salaam.

LOWASSA ALIKUWA MGENI RASMI KATIKA JUBILEE YA MIAKA 50 YA KANISA KATOLIKI MAHENGE


Mheshimiwa Edward Lowassa akiwasili kwenye sherehe hizo

JELA MWAKA MMOJA KWA KUMUOA BINTIYE WA MIAKA 11!

Waliobahatika kuwa shule ndo hao, wengine huanza shule ya awali wakiwa na miaka 11.
Wakati harakati mbali mbali za kukabiliana na ndoa na mimba za utotoni zikiendelea na hasa katika nchi za Afrika, baadhi ya nchi barani humo zinakabiliwa na changamoto hiyo kupita kiasi.

UTAFITI WAONYESHA KUWA NA WAPENZI WENGI NI TIBA YA SARATANI!

Kuwa na wapenzi wengi
Kulala na wanawake wengi kunapunguza hatari ya kupatikana na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo, kulingana na utafiti.

BOSI WA KAMPUNI YA APPLE ASEMA: NAJIVUNIA KUWA SHOGA!

Mkuu wa kampuni ya Apple Tim Cook
Mkuu wa kampuni ya Apple Tim Cook ametangaza jinsia yake akisema kuwa ''anajivunia kuwa shoga''.

HATARI KUBWA, BUNGE LA BURKINA FASO LACHOMWA MOTO


Burkina Faso

Waandamanaji nchini Bukina Faso wameteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, kupinga hatua ya kuongeza muhula wa Rais Blaise Compaore ambaye ametawala nchi kwa miaka 27.

ETHICS AND ANTI-CORRUPTION COMMISION ARRESTS 10 TRAFFIC POLICE OFFICERS IN NAKURU

Traffic police officers at work. Ethic and Anti-corruption Commission officials arrested 10 traffic police officers in Nakuru for allegedly receiving bribes from motorists. FILE PHOTO | NATION MEDIA GROUP 
By WANJIRU MACHARIA
Nakuru: The anti-graft agency Thursday conducted the biggest swoop in Nakuru and arrested 10 traffic officers for allegedly receiving bribes from motorists.

SHY-ROSE BHANJI ALIVURUGU BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Shy-Rose Bhanji. Picha na Maktaba 
Na Neville Meena, Mwananchi
Kigali. Kwa siku zaidi ya 10 sasa, Bunge la Afrika Mashariki (Eala) limeshindwa kuendelea na vikao vyake mjini hapa kutokana na wabunge wake kugomea vikao hivyo vya mkutano wa pili, wakishinikiza kuchukukuliwa hatua kwanza kwa mmoja wa wabunge wake, Shy-Rose Bhanji wa Tanzania.

AINA MPYA 27 ZA WANYAMA ZAGUNDULIKA TANZANIA



Na Florence Majani, Mwananchi
Profesa Neil Burgess, anayeongoza barani Afrika kwa utaalamu wa baioanuai na mwenyekiti mwenza wa TFCG, anasema milima ya tao la Mashariki imekuwa ikijulikana kwa muda mrefu kuwa na aina nyingi za viumbe ijapokuwa kumekuwa na ukosefu wa takwimu sahihi hasa katika maeneo sita kati ya 13 ya milima hiyo.

TANZANIA YAONGOZA KWA UZALISHAJI WA MPUNGA AFRIKA MASHARIKI


Na Kalunde Jamal, Mwananchi
Licha ya taarifa mbalimbali kuonyesha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wameajiriwa na sekta ya kilimo, hali ya sekta hiyo bado si ya kuvutia.

RUZUKU HATARINI KUKWAMISHA UKAWA!


Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi 
Na Boniface Meena, Mwananchi
Dar es Salaam. Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amesema Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unakabiliwa na changamoto kubwa suala la ruzuku.

MSIBA MZITO: ZAMBIA YAPOTEZA RAIS WA PILI AKIWA MADARAKANI!

Marehemu Michael Sata

Na Isaya Kisimbilu
Zambia imeendelea kukumbwa na mkasa wa kufiwa na marais wake wakiwa bado madarakani, baada ya Rais Michael Sata (77) kufariki dunia  jijini London, Uingereza alikokuwa amelazwa kwa  matibabu.

ICC YAMZUIA LAURENT GBABO KUMZIKA MAMAKE

Rais wa zamani wa Ivory Coast, aurent Gbabo
Majaji katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai na uhalifu wa kivita huko The Hague wametupilia mbali ombi la raisi wa zamani wa Ivory Coast kwenda kuhudhuria katika maziko ya mamake mzazi.

CHAMA CHA NIDAA CHASHINDA TUNISIA

Kiongozi wa Nidaa Tounes
Chama cha kidini nchini Tunisia Nidaa Tounes kimeshinda viti 85 katika uchaguzi wa ubunge nchini humo kulingana na matokeo.

HIACE YAUA WATU 12 ARUSHA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas

Na Asraji Mvungi, Arusha
Watu 12  wamekufa papo hapo na wengine wawili kujeruhiwa baada ya basi  dogo aina ya Toyota Hiace maarufu kama kipanya walikokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la mafuta.

HII SASA KALI: MUME MKOROFI AANDALIWA MLO WA KONDOMU!

Kondomu
Mwanamke mmoja mwenye watoto watatu katika wilaya ya kole nchini Uganda alimuandalia mumewe mlo wa mipira ya kondomu kufuatia ugomvi usiokwisha.

ADHABU KALI SIYO DAWA YA DAWA ZA KULEVYA

Mwaka 2013 Uruguay ilikuwa nchi ya kwanza kuruhusu kilimo cha bhangi
Taarifa ya utafiti wa serikali ya Uingereza umeilinganisha nchi hiyo na nchi kama Ureno, ambako kukutwa na kiasi kidogo cha dawa za kulevya kunaadhibiwa vikali.

MALINZI ATUMA RAMBIRAMBI MSIBA WA SATA, MEYIWA

Jamal Malinzi, Rais wa TFF

Na Mwandishi Wetu
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatumia salamu za rambirambi vyama vya mpira wa miguu vya Zambia (FAZ) na Afrika Kusini (SAFA) kutokana na vifo vya Rais Michael Sata na kipa wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini, Senzo Meyiwa.

KAMPENI YA TUSKER YAENDELEA KILIMANJARO, MWANZA

Meneja masoko wa Tusker Lager Anitha Msangi akiongea na wasambazaji wa biaza SBL  kwenye uzinduzi wa kampeni ya Tusker Fanya Kweli mjini Moshi.

TOYOTA ALLION INAUZWA, PIGA SIMU KWA MHUSIKA

TOYOTA ALLION
Mileage 100,000
CC 1800
Model; 2003
Ina mwaka na nusu tu nchini .
Kwa watakaohitaji piga simu

29 WAITWA KIKOSI CHA MABORESHO TAIFA STARS


Na Mwandishi Wetu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatarajia kuendelea na awamu ya pili ya maboresho ya timu ya Taifa (Taifa Stars) inayojumuisha vijana wenye umri chini ya miaka miaka 23.

MALI MPYA IMEWASILI



WASANII WAASWA KUWA NA NIDHAMU YA MUDA

Kiongozi wa Kundi la Kudansi la Wakali Sisi lililoshinda katika Shindano la Dansi mia mia hivi karibuni Yasin Haji (Kulia) akiongea na wadau wa Sanaa waliohudhuria kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii. Kushoto ni Afisa Sanaa kutoka BASATA, Ernest Biseko.

SDL KUANZA KUTIMUA VUMBI NOVEMBA 22


Na Mwandishi Wetu
Michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayoshirikisha timu 24 zitakazocheza katika makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini itaanza kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu.

TFF YAOMBA WADAU WABUNI JEZI MPYA YA TIMU ZA TAIFA


Na Mwandishi Wetu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linakaribisha wabunifu, kubuni mwonekano wa jezi mpya za timu ya Taifa kwa mechi za nyumbani na ugenini. Ubunifu ni lazima uzingatie rangi za bendera ya Taifa.

UMOJA WA MATAIFA YAINYUKA WIZARA YA MAMBO YA NJE BAO 3-0 KWENYE BONANZA LA UN FAMILY DAY

DSC_0176
Pichani juu na chini ni baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na watoto wa wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walipojumuika pamoja mwishoni mwa juma kushiriki michezo mbalimbali kwenye UN Family Day kusheherekea maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanishwa kwake.