Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 1 July 2016

CHANGAMOTO YA UONI HAFIFU KWA WATU WENYE ALBINISM


*ALBINISM AWARENESS FOUNDATION*
Watu wenye Ualbino(Albinism)  wanakabiliwa na changamoto ya Uoni Hafifu. Changamoto hiyo ya Uoni hafifu haiwezi kutatuliwa kwa 100% na miwani ya macho, Miwani inaweza kumsaidia kwa asilimia chache tu.
Changamoto ya uoni hafifu kwa watu wenye albinism inatokana na kutostawi vizuri kwa mishipa ya macho kunakosababishwa na upungufu au ukosefu wa rangi ya asili yaani *Melanin* kwenye macho.
Tatizo la uoni hafifu linatofautiana  kati ya mtu mmoja mwenye Albinism na mwingine. Ifahamike tu kwamba watu wote wenye Albinism wana changamoto ya uoni hafifu.
Pamoja na changamoto ya uoni hafifu inayowakabiri watu wenye albinism wanaweza kufanya mambo mengi ikiwemo kusoma maandishi,kutembea wenyewe,kuvuka barabara na baadhi yao kuendesha magari,pikipiki,baskeli,bajaji na vyombo vingine vya usafiri.
*Naomba jamii ifahamu kuwa Watu wenye Albinism hawatumii maandishi ya nukta nundu(braille) yanayotumiwa na watu wenye ulemavu wa kutoona(Visual Impaired)*
Nawaomba sana watanzania wenzangu mnisaidie  kusambaza Elimu hii kwa watu mbalimbali,makundi na mitandao mbalimbali ya kijamii, nina imani elimu hii ikiwafikia watu  kwa wingi na itasaidia jamii kuachana na fikra na mitazamo potofu inayopelekea vitendo vya Unyanyapaa, ukatili na mauji dhidi ya watu wenye Albinism.
 
Unaweza kupata elimu ya Albinisn kupitia mitandao ya kijamii kama vile facebook na 
twitter@suleimanmagoma na kupitia tovuti ya www.albinismtanzania.co.tz
Asanteni sana kwa kuniunga mkono. Mungu awabarik

No comments:

Post a Comment