Chama
cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers
Network' – TBN inawaomba wanachama wake wote kutotumia taarifa ama habari au
picha yoyote kutoka katika mkutano wa maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
(WPFD) unaofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
Kamati
Kuu ya Uongozi TBN imefikia hatua hiyo leo baada ya kujadiliana na kujiridhisha
kuwa kumekuwepo na taasisi za tasnia ya habari ambazo zimekuwa zikiwatenga
wanahabari wa mitandao ya kijamii (bloggers) na kutotambua umuhimu wao wakati
sehemu kubwa ya taarifa mbalimbali nchini husambazwa na mitandao hiyo.
TBN
iliyosajiliwa rasmi serikalini Aprili 2015 na kupewa namba ya usajili; S. A
20008 inawataka wanachama wake kutotoa ushirikiano wa sina yoyote kwa taasisi
ambazo zinawatenga bloggers.
Tunasikitika
kufikia hatua hii ila hamna jinsi. TBN itasikitika na kumshangaa mwanachama wake
au blogger asiye mwanachama kutounga mkono agizo hili, na kwenda kinyume na agizo
hili. Muda umefika ‘Bloggers’ kudai heshima, kutambulika na kuthaminika kama
tasnia ya habari ingine yoyote.
Imetolewa
na;-
Mwenyekiti wa Muda wa TBN
Joachim E. Mushi
03/05/2016
No comments:
Post a Comment