Sudan Kusini imetambuliwa rasmi na kamati ya kimataifa ya Olimpiki, na hivyo kuruhusu kushiriki katika Olimpiki mwakani, huko Rio de Janeiro.
Sudan Kusini ilipata uhuru miaka mine iliyopita, na hivyo haikuwahi tarehe ya mwisho ya kuweza kuingia katika Olimpiki ya London ya mwaka 2012.
Mkimbiaji wa Sudan Kusini, Guor Marial, alishiriki chini ya bendera ya Olimpiki.
Wawakilishi wa Sudan Kusini walitokwa machozi, nchi yao ilipokubaliwa kuwa mwanachama wa Olimpiki ( na kuwa mwanachama mia mbili na 6).
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment