Mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete akitoa
hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
alioizindua Kitaifa jijini Tanga leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni
“Endesha Salama Okoa Maisha”. Katika hotuba yake, Rais Kikwete aliwataka
Wajumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani wabadili mfumo walionao kutoka Analogi
kwenda Digitali ili mfumo huo uweze kupunguza rushwa pamoja na ajali nchini. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Washiriki wa maonesho wakiwa katika
maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa
katika Kiwanja cha Tangamano, jijini Tanga leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya
mwaka huu ni “Endesha Salama Okoa Maisha”. Katika hotuba yake, Rais Kikwete ambaye
ndiye aliyefungua maandamano maadhimisho hayo, aliwataka Wajumbe wa Kamati ya
Usalama Barabarani wabadili mfumo walionao kutoka Analogi kwenda Digitali ili
mfumo huo uweze kupunguza rushwa pamoja na ajali nchini. Picha
na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Washiriki wa maonesho ambao ni wanafunzi
wa shule za msingi jijini Tanga wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe usemao ‘Sote
tuna Haki ya Kutumia Barabara’, kundi hilo la wanafunzi hao ambao ni moja ya makundi ya waandamanaji
wakiwa wanapita mbele ya jukwaa la mgeni rasmi, Rais Jakaya Kikwete (hayupo
pichani) ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa wiki hiyo. Rais Kikwete ambaye ndiye
aliyefungua maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama jijini humo, aliwataka
Wajumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani wabadili mfumo walionao kutoka Analogi
kwenda Digitali ili mfumo huo uweze kupunguza rushwa pamoja na ajali
nchini. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani nchini, Pereira Ame Silima akitoa hotuba yake kabla ya
kumkabirisha mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete kuja kutoa hotuba yake ya ufunguzi
wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambapo kwa mwaka huu imebeba kauli mbiu
ya “Endesha Salama Okoa Maisha”. Katika hotuba yake, Silima aliwataka madereva
nchini kufuata sheria za barabarani ili waweze kuepuka ajali ambazo nyingi
zinasababishwa na uzembe wao. Picha na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshika
sanamu lenye kuonyesha mtu akiwa anavuka barabara katika eneo la kivuko cha
waenda kwa miguu katika Banda la Maonesho la Usalama Barabarani wakati wa
Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliozinduliwa na Rais
Kikwete, jijini Tanga leo. Katika hotuba yake kabla ya kuyazindua maadhimisho
hayo, Rais Kikwete aliwataka Wajumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani wabadili
mfumo walionao kutoka Analogi kwenda Digitali ili mfumo huo uweze kupunguza
rushwa pamoja na ajali nchini. Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Pereira Ame Silima, kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani,
Kaimu Kamishna wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamedi Mpinga. Kushoto ni
Trafiki kutoka Makao Makuu Dar es Salaam, Meja Enock Machunde. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Wananchi mbalimbali na wageni waalikwa
wakiwa katika harakati ya kuingia katika mabanda mbalimbali katika Kiwanja cha
Tangamano, jijini Tanga mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzindua Wiki ya
Nenda kwa Usalama Barabarani jijini humo. Kauli mbiu ya mwaka huu ya
maadhimisho hayo ni ‘Endesha Salama Okoa Maisha’. Rais Kikwete katika hotuba
yake ya ufunguzi amewataka Wajumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani wabadili
mfumo walionao kutoka Analogi kwenda Digitali ili mfumo huo uweze kupunguza
rushwa pamoja na ajali nchini. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Rais Jakaya Kikwete akikata utepe ikiwa
ni ishara ya kuzindua reflector mpya za kubandikwa kwenye magari nchini ili
ziweze kuzuia ajali. Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Pereira Ame Silima, na kushoto ni Kamishna wa Kikosi cha Usalama
Barabarani, Jeshi la Polisi, Mohamedi Mpinga. Rais Kikwete alizindua Wiki ya
Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo kitaifa inafanya katika Kiwanja cha
Tangamano, jijini Tanga. Katika hotuba yake, Rais Kikwete aliwataka Wajumbe wa
Kamati ya Usalama Barabarani wabadili mfumo walionao kutoka Analogi kwenda
Digitali ili mfumo huo uweze kupunguza rushwa pamoja na ajali nchini. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Waendesha pikipiki (bodaboda) pia
walishiriki kikamilifu katika uzinduzi wa maonesho hayo yaliyofanyika katika
Kiwanja cha Tangamano jijini Tanga leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu
ni “Endesha Salama Okoa Maisha. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO
CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
No comments:
Post a Comment